#COVID19 Tahadhari: Usifue “surgical mask” wala N95; za kitambaa zifuliwe na kupigwa pasi

#COVID19 Tahadhari: Usifue “surgical mask” wala N95; za kitambaa zifuliwe na kupigwa pasi

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, ‘surgical masks’ na mask aina ya N95 hazipaswi kufuliwa wala kuvaliwa zaidi ya mara moja. Baada ya matumizi, ikiloa au kila baada ya saa 4, mask ivuliwe kwa umakini na kutupwa

Mask inapofuliwa, inapoteza ubora wake na hivyo kuathiri uwezo wa awali wa kuzuia unyevu kutoka au kuingia kwa sababu malighafi yake haihimili ufuaji

Barakoa za kitambaa zifuliwe na kupigwa pasi kila zinapovuliwa ili kuua vijidudu vyovyote. Ni vyema ukawa na barakoa za kitambaa zaidi ya moja ili kurahisisha ufuaji na kuhakikisha inakauka vyema

Usitoke nje ya nyumbani kwako bila barakoa. Kumbuka kuvaa barakoa si mbadala la kunawa kwa maji tiririka na sabuni au kitakasa mikono

#JFCOVID19_Updates #Barakoa
C09E2267-B428-4AFA-B8E5-CF7911AE2E0B.jpeg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom