TAHADHARI: Wagonjwa wa Kisukari, Moyo, Shinikizo la Damu na Saratani wako hatarini zaidi wakiambukizwa #COVID19

TAHADHARI: Wagonjwa wa Kisukari, Moyo, Shinikizo la Damu na Saratani wako hatarini zaidi wakiambukizwa #COVID19

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) inaeleza kuwa tafiti zilizofanywa katika Mataifa yenye Wagonjwa wa #CoronaVirus watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Kisukari na shinikizo la damu kuwa katika hatari zaidi wanapoambukizwa #COVID19

Imefafanuliwa kuwa magonjwa haya kwa kiasi kikubwa huathiri kinga ya mwili ambayo inaweza kupambana na Virusi vya Maginjwa mbalimbali ikiwemo Corona

WHO inaeleza kuwa watu wenye changamoto za magonjwa haya na mengine mengi yanayohusisha kushuka kwa kinga ya mwili wanapaswa kuwa waangalifu zaidi dhidi #CoronaVirus

Inashauriwa kuwa kupuka mikusanyiko, ukiweza kaa nyumbani, nawa mikono kwa sabuni na maji tiririka. Endapo utaona dalili za maambukizi, tafadhali wasiliana na mamlaka ili upatiwe ufumbuzi
 
Upvote 0
Most of them wapatikanapo huko CCM. Rest in Peace in advance

"My pain may be the reason for somebody's laugh,but my laugh must never be the reason for somebody's pain"

Charlie Chaplin
 
HIYO REPORT SI KITU CHA KUZINGATIA SAANA, KWA SABABU KILA MTU AMESHAPANGIWA ATAISHI MUDA GANI NA SABABU YA AJALI YAKE PIA IMESHAPANGWA. TUSITISHANE
 
Mungu atusaidie wote kwa pamoja. Tulivuke janga hili.
 
HIYO REPORT SI KITU CHA KUZINGATIA SAANA, KWA SABABU KILA MTU AMESHAPANGIWA ATAISHI MUDA GANI NA SABABU YA AJALI YAKE PIA IMESHAPANGWA. TUSITISHANE
Hili ndio neno!Jitu linakurupuka kutoka wapi sijui huko inantaka kutisha watu hapa
 
Kumbe hata huyu msanii wetu aliyeugua naye inawezekana alishaunganishwa kwenye gridi ya taifa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom