Tahadhari: Wanawake wengi hatarini kukamatwa/kufungwa. Tujulishane hili

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Kutokana na TAKUKURU kuonekana wamepewa meno kukamata wanaotaka rushwa na pia watoaji. Kuna hatari kubwa ya wanaume na wanawake wengi kukamatwa.

Tunajua jinsia ambavyo wadada wengi wamekuwa hawakubali kutoa penzi mpaka wapewe rushwa jambo hili limeonekana luwa linaleta changamoto kwa maskini kupata mapenzi.

Katika kuangalia suala la usawa katika mapenzi tunausia TAKUKURU kuangalia wanawake wanaopokea rushwa ili wakubali mahusiano ya kimapenzi lakini pia na wanaume wanaotoa rushwa nao wakamatwe bila kuwaonea haya.

Imekuwepo tabia ya wanawake kutotaka kutoa penzi mpaka wapate zawadi au pesa, hili jambo ni ukiukwaji wa haki za binadamu kama ambavyo sasa hivi tunapiga kelele wagombea ubunge na udiwani kugawa rushwa.bas na TAKUKURU pia imeamua kulivalia njuga suala hili la rushwa katika mapenzi.

Na watu wengi watafungwa au wataenda motoni wakifa sababu hata vitabu vinakataza kutoa na kupokea rushwa, nawausia dada zangu msikubali kupokea pesa au kitu ili ulainike na kuachia penzi, usikubali kamwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…