Tahadhari: Wizi mpya kwa wenye magari

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
10,400
Reaction score
14,339
Kuna wizi mpya umeingia, mjini haswa kwa wenye magari yanayotumia remote control.

Nadhani wataalamu wameshatengeneza remote yenye kuweza kuingiliana na remote nyingine hivyo kwa sasa remote za magari sio salama hata kidogo.



Kinachofanyika haswa sehemu za parking za public, kwenye parking yenye msongamano wa magari mengi, pengine kuna walinzi lakini tukumbuke kuwa mlinzi au walinzi hawawezi kukariri kila gari na mmiliki wake.

Nadhani wezi hao wapo kwenye majaribio ya wizi wao huo mpya kwani shida yao inaonekana kuwa sio kuiba magari bali ni kuiba kilichopo ndani ya magari.



Mwizi mwenye remote inayofanana na remote ya gari fulani, baada ya kuona kwenye magari hakuna mtu, ataibonyeza remote yake kisha gari yoyote itakayoitika itakuwa ndio windo la huyo mwizi, remote ndio kila kitu kwenye gari, remote inaweza kuwasha gari, kufungua milango yote na pengine kufungua boneti zote za gari.

Gari ikifanikiwa kuitikia baada ya mwizi kubonyeza rimoti yake. Mwizi ataisogelea gari husika kwa tahadhari kisha anafungua mlango wa dereva ambako mara nyingi kuna vitu vya thamani vitakuwa vimeachwa.



Chimbuko la wizi huu ni huko UK, Marekani, wenzetu wameshajifunza jinsi ya kujikinga na aina ya wizi huu wakaona kuwa remote hazina maana kabisa.

Hivyo kuwa makini kabisa unapoacha gari lako kwenye public parking na ikiwezekana ni bora kabisa ukafunga gari kwa funguo tu ama ukahakikisha unamuacha mtu ndani ya gari. Au kutokuacha vitu vya thamani ndani ya gari.
 
Mimi gari langu nikifunga na funguo bado naweza kufungua na remote, hapo vipi...dawa ni kukaa humo humo na kuanza kuagiza vitu kimoja baada ya kingine, au ni kuondoa kabisa alarm kwenye gari
 
Mimi gari langu nikifunga na funguo bado naweza kufungua na remote, hapo vipi...dawa ni kukaa humo humo na kuanza kuagiza vitu kimoja baada ya kingine, au ni kuondoa kabisa alarm kwenye gari
ondoa alarm tu...maana mtu akibonyeza rimoti hatokuwa na haja ya funguo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…