Hii Ni tahadhali Kama ilivyotolewa na uongozi wa JF;
"Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS"
Ningependa neno "kuosha" libadilike na kuwa "kunawa". Tahadhari Isomeke hivi;
"Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kunawa mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS"
Neno kuosha linatumika zaidi Kwa Maiti ndo ule msemo wa "Mwosha huoshwa" ukawepo na Ile mwingine "Siri ya Maiti aijua Mwosha"