Tahadhari ya ushirikina kwenye biashara yangu

SHAIDI

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2014
Posts
291
Reaction score
141
Wana jf, katika harakati ya kjikomboa kiuchimi nilifikiri kuanzisha biashara ya kuuza chipsi maeneo ya tabata, niko kwenye mchako wa kutafuta location na nimepata kwa taadhari ya kwamba hapo nilipopata kuna watu walishafanya hii biashara lakin baada ya kipindi biashara inakufa nilitaadharishwa hivyo na muhusika, me kama mdogo wake na ni vizuri akaniambia ukweli kuna mambo ya kishirikina maeneo hayo kwa sababu kuna wafanya biashara wengine lakin sio wa biashara kama hii ya chipsi

Mimi binafsi nilishtuka lakin nikajikaza kiume nikamwambia kuwa nitaichukulia kama changamoto, leo jioni ndiyo nataka kwenda kulipia lakin nasita kwa tahadhari niliyopewa, location ni nzuri sana bei nafuu, ndugu zangu me namwamin mungu nikijua kwamba kuna shetan(ushirikina)
naombeni ushauri kuhusu hili je nilipe hiyo pango? au nitafute shemu nyingine?
na nikilipa nifanye nini kuepuka hii tahadhari niliyopewa?
natanguliza shukrani,
 
kalipe mkuu acha uoga ,,,,nakuhahakishia km kweli una imani na mungu biashara yako itafanikiwa


 
Nenda ukalipie.....ila kabla hujaanza biashara hapo..kulingana na dini yako hakikisha unapafanyia maombi.......
 
Bado iman yako ni haba, we si umesema unamwamin mungu au
 
Shetani wa vigangula wametapakaa dunia nzima, labda biashara yako ukaifanyie kuzimu
 
Cyberteq unanifurahisha sana comment zako.
Umempa ushauri mfupi na wakueleweka lakin una maana kubwa ndani yake.
Kweli jamaa kasharogwa hatoweza tena hiyo biashara hapo mpaka pale atakaposema kwa moyo wa dhati kwamba naweza na ntafanikiwa kwa kupanga mikakati madhubuti na kufanya kazi kwa nguvu zote pamoja na ubunifu wa kufa mtu. Vinginevyo ndio basi tena!!!
Ole wako umsahau Mungu.
 
Bora hao washirikina ni nafuu kuliko hao Madem utakaowahonga hako kamtaji ukianza biashara.

Muamini mungu na umpe nafasi yake na yeye atakulinda.
-Yeye ndie mwenye uhai wa Maisha uliokamilika
-Yeye ndie msimamizi wa Kila jambo
-Wala hashindwi kuvilinda vyote vilivyomo ardhini na mbinguni,vinavyoonekana kwa macho na visivyoonekana kwa macho
-Yeye ndie aliejuu ya kila kitu na ndie Mkuu kabisa
(Qur`an :2:55 - Ayatul-Kursi)
 
Acha uoga,mkabidhi Mungu njia zako zote naye atanyosha mapito yako,hakuna sehemu salama kila mahali pana changamoto zake,lakini Mungu akiwa kiongozi wako na ukafanya bidii katika kazi yako hakika utafanikiwa.
 
amina , nashukuru kwa kunipa moyo, nitarudisha feedback nimefikia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…