Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Pombe siyo kwenye maji kuna mshikaji alikuwa moja ya taasisi inayohusika na mafunzo ya baharini alitoweka.Namba 3 hapo sikuungi mkono kabisa kwingine kote umepatia ila #3 ni vice versa
Hongera Sana Bujibuji simba Nyamaume kwa kuleta uzi mzuri sana.ππ»
Kuogelea ni burudani nzuri, lakini maji yanaweza kuwa hatari usipochukua tahadhari. Kwa usalama wako, zingatia haya:
1οΈβ£ Usiogelee sehemu usiyoijua kina chake au ambayo haijaandaliwa kwa ajili ya kuogelea.
2οΈβ£ Hakikisha kuna mlinzi wa kuogelea (lifeguard) ikiwa unaenda kwenye bwawa au eneo la kuogelea la umma.
3οΈβ£ Usiogelee ukiwa umelewa pombe au umetumia kitu kinachopunguza uwezo wako wa kufanya maamuzi.
4οΈβ£ Usiogelee peke yako. Ukiwa unaogelea, mwambie mtu au kaa karibu na watu wengine.
5οΈβ£ Watoto wasiachwe peke yao karibu na maji, hata kama wanaonekana wanajua kuogelea.
6οΈβ£ Usikimbie pembeni mwa bwawa, kwa sababu sakafu inaweza kuwa na utelezi na kusababisha kuanguka.
7οΈβ£ Usisukume au kumtupa mtu mwingine majini kama mzaha. Maji si sehemu ya kufanya mizaha ya hatari.
8οΈβ£ Kabla ya kuingia majini, angalia alama za tahadhari na fuata sheria za eneo hilo.
9οΈβ£ Epuka kuingia baharini wakati mawimbi ni makubwa au kuna tahadhari ya hali mbaya ya hewa.
π Usiingie majini ukiwa umechoka sana au unapojisikia dhaifu.
1οΈβ£1οΈβ£ Ukiwa hujui kuogelea vizuri, tumia vifaa vinavyofaa vya kujikinga na kaa kwenye kina salama.
1οΈβ£2οΈβ£ Ukiona mtu anazama, usiruke majini bila ujuzi wa uokoaji. Tafuta msaada wa lifeguard au watu waliofunzwa kuokoa maisha.
NB: Kumbuka...
ππ» Maji yanaweza kuonekana tulivu lakini yakawa na hatari.
ππ» Usalama wa maji unaanza kabla hujaingia majini.
ππ» Furahia kuogelea, lakini usiidharau nguvu ya maji.
"Maji ni burudani ukiyaheshimu, lakini yanaweza kuwa hatari ukipuuza tahadhari." πππΎββοΈ
Wewe unatoka Mwakaleli!!!!ππ»

NdituWewe unatoka Mwakaleli!!!!
Ku ilisu ipimbaWewe unatoka Mwakaleli!!!!
Mungu akutunze broHongera Sana Bujibuji simba Nyamaume kwa kuleta uzi mzuri sana.
Mkuu mimi bila kujikwatua siogeleiPombe siyo kwenye maji kuna mshikaji alikuwa moja ya taasisi inayohusika na mafunzo ya baharini alitoweka.
Duh basi upo fresh mzee wa kazi, mimi nikiwa na hivyo vitu nimevitandika marufuku kabisa hasa ziwani ndiyo hapana.Mkuu mimi bila kujikwatua siogelei
Hata ukijua kuogelea kuna kubanwa na msuli ndiyo maana akaandika usiogelee peke yako. Msuli ukikushika kama huna msaada tunakuzikaHili bandiko lako ni kwaajiri ya wasiojua kuogelea, maana tahadhari ni nyingi mno, Hofu ni kubwa mno maji asili yake kadri unavyokuwa na hofu kubwa ndivyo yanavyo kumaliza fasta, tahadhari no 3,7 na 10 ziko poa sana,
jambo lingine la muhimu ni lazma ujue stamina yako unaweza ogelea kwa umbali gani bila shida yoyote
Pia wale wapenda matyubu ya gari yanasaidia kwa kiasi kikubwa
ila upepo ukivuma kwa kasi linaweza kukupeleka kwenye kina kirefu zaidi au likatereza mikononi mwako shida ikaanzia hapo
Ikitokea umepelekwa mbali na tyubu kwa sababu ya upepo mkali na huwezi kuogelea umbali mrefu omba msaada lakini usiliachie