Tahadhari za kuzingatia kwa watu wanaokwenda kwenye mkesha wa chako ni chako Kawe

Tahadhari za kuzingatia kwa watu wanaokwenda kwenye mkesha wa chako ni chako Kawe

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Ni tahadhari tu,

kutokana na wingi wa watu leo lazima kenge wamo ingawa ni vigumu kuwajua. Kwa wale mnaoenda mkesha wa chako ni chako kawe leo:

1. Usalama wako uanzie kwako mwenyewe.

2. Ukiwa na begi lolote usiamini mtu wa pembeni yako.

3. Unapoenda haja hakikisha uko na begi zako.

4. Ukiona kuna mtu amekubana sana mara kwa mara kuna polisi jamii watakuwa around jitahidi kuwajulisha mapema.

5. Usikubali kula kitu unachopewa na mtu usiemjua kwenye mkesha.

6. Unapotoka asubuhi ya mapema kuanzia saa kumi muwe kwenye group.

7. Wale wenye watoto mjitahidi saana saana kuwa nao karibu kwani kuna upotevu wa watoto hutokea isijekuwa wako.

8. Unapopanda basi hakikisha kama ni pochi yako iko mfuko wa mbele kwa wamama ikumbatie kabisa wakikukosa uwanjani wanakupiga kwenye basi usije sema huna nauli umejimaliza kumbe wameshafanya yao.

Nakutakia mafanikio mema unaekuja na utakaekuwa ukiangalia kwenye tv ama youtube, distance isnt a barrier, upako ufike popote.

Mungu awape haja ya mioyo yenu wapendwa.

App Pdidy
 
Back
Top Bottom