Shimilimana
Member
- Mar 12, 2013
- 52
- 15
Salute wana Jf wote: Baada ya kuwa nimefuatilia kwa muda mrefu namna ya hii mitandao ya kuuza bidhaa za tiba lishe/food supplements/food dietary, nimegundua kuwa tiba lishe kama ilivyo haina tatizo bali wasambazaji wake ndiyo wenye tatizo. Mojawapo ya tatizo kubwa nililoliona ni kwa wale wasambazaji wanaomcha Mungu, nimegundua ni wengi sana kama siyo robo tatu ya wote ambao ndiyo hasa nimesukumwa kuwapa tahadhari kwa hiki wanachokifanya. Baada ya kuahidiwa utajiri kwa kushawishi watu kujiunga na mitandao hii, wanatumia nguvu nyingi ikiwemo uwongo ili kuwavuta watu kujiunga na mitadao hii badala ya kutumia nguvu hiyo na ukweli kuwafanya watu wamche Mungu ili wapate utajiri usiyo na mwisho wala majuto. Mwenye kuelewa na aelewe, tubadilike ili tuepuke hasira ya Mungu baada kuwa tumeondoka hapa dudiani na kuuacha utajiri huu wenye hila. Thanks, be blessed