TAHARIRI: Wajumbe, hamjaenda bungeni kupiga porojo na 'kuula'. Ni kutengeneza katiba mpya!

TAHARIRI: Wajumbe, hamjaenda bungeni kupiga porojo na 'kuula'. Ni kutengeneza katiba mpya!

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Hatimaye bunge maalum la katiba linaanza leo.Hili ni bunge ambalo kwa namna moja au nyingine litatoa mawazo ambayo yatapelekea kupatikana kwa katiba mpya ya Watanzania wote.Katiba ya sasa imepitwa na wakati mno huku ikivunjwa kwa makusudi na viongozi wakuu wa serikali kutokana na uchovu wake.

Sisi Watanzania tulio nje ya bunge hilo tunatarajia kuwa kitakachojadiliwa ni kutafuta mifumo sahihi ya kiutendaji kutokana na maoni ya tume ya Jaji Warioba na sio kuleta maoni mbadala kutokana na msukumo wa chama fulani cha siasa au kikundi cha watu.Kwa mfano tume ilipendekeza serikali tatu kutokana na maoni ya Watanzania wengi,ni jukumu la bunge hili kutafuta muundo utakaofaa na kukidhi mahitaji kutokana na hizo serikali tatu na sio kuanza kupendekeza maoni yaliyotolewa na kamati kuu ya CCM.Maoni ya kamati kuu ya CCM yalitolewa na Watanzania wachache sana chumbani Dodoma ili kukidhi ubinafsi wao! Hayo hayakubaliki kamwe!

Ni wakati wa bunge hili kutumia akili na uzalendo wa hali ya juu kujadili.Hatutaki kuamini zile fununu eti baadhi ya wajumbe mufilisi wa hoja waliandaliwa hoja za kujibu kutoka kwa Evod Mmanda (mwanasheria na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM), Dr. Asharose Migiro na wana CCM wengine ndani ya bunge la katiba!

Tunahitaji katiba itakayoelezea kila kitu bayana,kutambua haki muhimu za binadamu,kutambua majukumu ya watendaji muhimu nchini na kuwawajibisha vilivyo wahuni na wazembe bila kujali cheo cha mtu.Tunahitaji katiba itakayo heshimiwa na wote.

Sisi tulio nje tupo tayari kupambana na wote watakaoendekeza maslahi binafsi ndani ya bunge hilo.Tupo tayari kwa hilo!

Asanteni na kila lakheri kutetea maslahi ya Watanzania wengi.

Mods naomba msihamishe uzi huu!
 
Katiba mpya ipi tena wakati Rais, Makamu wake,Waziri Mkuu, Mwanasheria mkuu, Mawaziri,Manaibu Waziri,Wabunge wote wa ccm pamoja na viongozi wote wa ccm Taifa wameshatoa msimamo wao ni kuweka VIRAKA TU.
 
Kwa wateule wa Rais, sina shaka nao. Labda hawa wa kuchaguliwa kama akina Lema, Sugu, Msigwa nk
 
Katiba mpya ipi tena wakati Rais, Makamu wake,Waziri Mkuu, Mwanasheria mkuu, Mawaziri,Manaibu Waziri,Wabunge wote wa ccm pamoja na viongozi wote wa ccm Taifa wameshatoa msimamo wao ni kuweka VIRAKA TU.
Nawapongeza ccm kwa kuliweka hilo wazi. Hata CHADEMA nao wameweka msimamo wao. Wengi wape
 
Hivi huo mjadala wa kushirikisha watu mia 6 na zaidi utafanyikaje?suppose kwa siku zote 70 kila mjumbe akichangia dakika 10 jumla ni dakika 7000 ,kama kwa siku wakikaa kwa masaa 8 ni takribani dakika 480 ambazo akti ya hizo 180 ni za speaker kuongea na kutoa miongozo,dakika 100 za kugonga meza na matangazo mengine,dakika 200 ni za kuchangia hoja na kubishana.Hivyo muda unaobaki kwa siku kuchangia ni kama dakika 100 ambazo zitahitaji siku 70 hivi ili kuwezesha angalau kila mjumbe kuongea.
 
Back
Top Bottom