Hali ni tete muda huu katika mitaa ya Kibera baada ya makundi mawili yaishio eneo hilo kuzozana juu ya maandamano yaliyoshuhudiwa mchana kutwa jijini Nairobi.
Kikundi kimoja kinasadikiwa kutoshiriki katika maandamano kikidai kuwa vuguvugu halitakuwa na natija mwisho wa siku, huku kikundi cha pili kikidai kuwa wananchi wanakumbwa na matatizo sawa ya kiuchumi na hivyo basi haiwezekani baadhi ya watu wakajitenga na maandamano.
Mzozo huo umepelekea Msikiti ujulikanao kama Al Aqsa eneo la Kibra kuteketezwa kwa moto(japokuwa moto ulidhibitiwa na waumini), lakini pindi baada ya kuzima moto vurugu za kulipa kisasi zikazuka na duru za kuaminika zinasema kanisa la PCEA Kibra nalo limeteketezwa kwa moto.
Hayo ni maneno ya wanasiasa tu!!pasipo na haki/ penye njaa ni ngumu sana kuilinda amani!!masikini huwa anaona hana cha kupoteza hata nchi ikiingia vitani!!mizozo mingi ya nchi za kiafrika hutokana na kundi kubwa la wananchi kuwa kwenye umasikini mkubwa.