Tahmeed vs Modern Coast vs Dar Express

Tahmeed vs Modern Coast vs Dar Express

Swahili_Patriot

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
358
Reaction score
831
Screenshot_20211104-150324_Chrome.jpg
Screenshot_20211104-150337_Chrome.jpg
Screenshot_20211104-150402_Chrome.jpg
 
Nimeshindwa kuattach ujumbe wangu kwenye heading but bora ujumbe ufike.
Kwa miaka ya nyuma kidogo about 2010-2016 basi la dar express limekuwa Kinara wa meendo na starehe sio ya kitoto. Ila kadri muda ulivyozidi kwenda, yamepoteza comfort yake kutokana n kuchakaa lakini mwendo wake umekuwa sio wa kitoto. Kwani, tangu nilijue dar express, cjawahi kushuhudia gari lolote lililowahi kutia nanga Nairobi mbele yake ijapokuwa kulikuwa n mabasi mengi yaliyopita route ya dar Nairobi kama spider n taqwa(kampuni imekufa kwa sasa), modern coast, saibaba n tahmeed. Hadi hivi sasa mabasi yote yanayonda route ya Nairobi hakuna basi lolote lililoweza kuliacha au kuachieve hata kufika mpakani mbele ya dar, ndio maana ninaamini kile chuma sio mchezo wallahi.
Kwa miaka ya 2014-18 ilikuja kampuni ya modern ambayo luxury yake ilikuwa next level. Hawa hawakujali kabisa kuhusu mwendo wa kiushindani ila walituguarantee wateja wake mwendo mzuri n starehe ambayo sidhani kuna basi lolote lililowahi kupita njia hio liliweza kulipiku. Lilipiga route kwa muda mfupi n kusitisha kabisa route ya dar nai.
Kwa sasa*kabla ya bro corona kuja, tahmeed ndio amekuwa mfalme wa starehe n mabasi nadhifu katika hio route ya dr nai. Ni mabasi yenye starehe ya kipekee, mwendo mzuri n kiukweli ninaipenda sana hii kampuni kwa quality services wanazozitoa.
Kwa uzoefu wangu wa kuyachanganua haya mabasi kadri macho yangu yanavyoweza kuyaona, imefika kipindi sasa nimekuwa n tamaa ya kutaka kujua kiundani kidoogo haya mabasi kiufundi zaidi. Kwa yeyote mwenye uzoefu wa kutosha, naomba mtupe darasa kuhusu ubora wa haya mabasi kiufundi zaidi n mnifafanulie kwanini dar express amekuwa bully kwa zaidi ya mlongo mmoja katika hii route. Asanteni
 
Back
Top Bottom