Richlifepaul_
Member
- May 26, 2024
- 5
- 5
Tanzania ilipata uhuru wake Tar 9 Desemba 1961, wakati huo ikijulikana kama Tanganyika. Zanzibar ikapta uhuru tar 9 Desemba 1963, na nchi hizi zikungana tar 26 Aprili 1964 kutengeneza nchi iitwayo Tanzania. Pamoja na kupata uhuru mapema lakini bado nchi haijaendelea vya kutosha, zipo sababu zilizopelekea kutokupata maendeleo mapema kulinganisha na nchi zilizopata uhuru baada ye Tanzania.
Sababu hizo nikama zifuatazo, Mfumo wa siasa na uchumi (ujamaa), mfumo huu uliweka ili kuwe na usawa na maendeleo, ulisababisha taifa kuwa na uchumi uliodhibitiwa sana na serikali, na kuzuia sekta binafsi kushamiri. Mfumo huu umesababisha ukuaji wa polepole wa uchumi kwa miaka mingi.
Miundombinu duni, nchi bila barabara, reli, na huduma za msingio za kijamii kama elimu na afya zilizo bora unaathiri sana uwezo wan chi kujiletea maendeleo. Kama kuna uduni wa miundombinu unapelekea kufukuza wawekezaji hasa wan je.
Ufisadi uliokithiri, hili ni kati ya m atatizo sugu nchini, ambalo linaathiri karibu kila nsekta ya uchumi wa nchi. Matumizi mabaya ya rasilimali za umma na fedha yamesababisha miradi mingi ya maendeleo kutokamilika au ikikamilika inakuwa chini ya kiwango.
Elimu na ujuzi, miaka mingi elimu ya Tanzania inaonekiana kutoendana na soko halisi la ajira hasa katika ujuzi unaotakiwa na soko la ajira. Ingawa kumekuwa na juhudi za kutatua na kuboresha elimu, bado kuna changamoto kubwa katika kuhakikisha kuwa nguvua kiazi ya nchi ina ujuzi na elimu inayohitajika kwenye soko la ajira la kisasa. Hii ijnapunguza nchi kuvutia wawekezaji katika sekta ya tehama na viwanda.
Siasa tulivu, japo kimataifa Tanzania inaonekana kuwa na siasa tulivu ikilinganisha nan chi zingine za Afrika, mara kadhaa kuna kuwa na migogoro isiyoisha inayoweza kuzuia maendeleo, mfano vyama vya siasa kunyimwa haki yao ya msingi ya kufanya mikutano, kuwepo na chaguzi zenye ushindi wa mashaka.
Kilimo (uchumi wa kilimo) na viwanda, Tanzania uchumi nwake umekuwa ukitegemea sana kilimo ambcho kwa hali ya kushangaza ni kilimo cha kujikimu zaidi na kinaathirika na mabadiriko ya hali ya hewa. Sekta ya viwanda bado inasuasua haina nguvu ya kuchangia sana kwenye ukuaji wa uchumi wa taifa.
Kulingana na changamoto hizo, Tanzania bado inasafari na kazi kubwa ya kuimarisha sera zake za kiuchumi na kijamii ili kifikia maendeleo yaliyo imara na ya haraka na yatakayokuwa endelevu kama nchi zingine. Kuna hatua mbalimbali zinaweza chukuliwa na Tanzania kuwa nchi tajiri, hatua hizo ni;
Kuboresha miundombinu, kuimarisha nishati ya umeme, barabara, reli, na bandari ili kuvutia wawekezaji, kukamilisha ujenzi wa miundombinu hii kwa wakati na kuhakikisha inajengwa ktk viwango vinavyotakiwa na sio kulipuliwa, ihakikishe mianya ya pesa ya umma kuliwa na watu wachache inatokomezwa ili nchi ipate miundombinu iliyoimara, lakini pia kuhakikisha miundombinu ya kimkakati inajengwa vyema kiuepusha ujenzi wa ovyo kama ule wa kuweka kituo cha mabasi ya mwendokasi pale jagwani.
Kukuza sekta ya viwanda, serikali inapaswa kuendeleza na kuimarisha uwekezaji kwenye sekta ya viwanda. Hii inaweza kufanyika kwa kutoa motisha kwa wawekezaji, kuboresha sera za biashara na kuanzisha maeneo maalumu ya viwanda. Kama nchi inatakiwa kuwaendeleza vijana wabunifu ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo nafuu, kuwapeleka kusoma na kuwapa miongozo pamoja na nakuwapa maeneo wajenge viwanda vyao. Pia kuwatafutia masoko nje ya nchi au kuwatafutia wabia ili vijana hawa ubunifu wao usife katika mikono yao. Serikali isitengeneze mazingira ya kuwakatisha tamaa vijana bali kuwajengea mazingira wezeshi ili kupanua sekta ya viwanda na ubunifu.
Kuboresha elimu na mafunzo ya ufundi, nguvu kubwa kwa sasa iwekwe kwenye elimu ya ujuzi ili vijana wapate maarifa na ujuzi unaoendana na soko la kazi. Serikali iwekeze katika mafunzo vitendo zaidi, kwasasa taifa lina wimbi mkubwa wa vijana wa elimu ya juu wasio na ajira, ni vyema kuimarisha vyuo na shule maalumu zitakazotoa elimu ujuzi kwa vijana, hii itaimarisha sekta mbalimbali na kuongeza ubunifu zaidi.
Kupambana na ufisadi/rushwa uliokithiri, serikali kama haitopambana na walafi wa rasilimali za umma hakutokuwa na uwajibikaji, viongozi walafi hawatakiwi kuwa maofisini. Ni juukumu la vyombo vyenye mamlaka husikja kuhakikisha inapinga ufisadi na sio wao haohao kuwa mafisadi. Serikali inatakiwa kuwawajibisha mafisadi ote, mfano katika ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali kunaonekana kuwepo na mianya mingi ya pesa umma kupotea lakini hakuna taarifa kama wahusika wamewajibishwa. Kama rasilimali za umma zitaishia kwenye mikono ya viongozi waovu basi itatuchukua miaka 100 kuona maendeleo, ni vyema viongoji wajue wajibu wao na sio kuiba.
Kukuza biaashara ndogo na za kati (SMEs), kuwasidia wafanyabiashara wadogo na wakati kwa kutoa mikopo nafuu, mafunzo ya biuashara, na kuwajengea uwezo wa kuingia kwenye masoko mapya, sambamba na hayo pia kuwepo na kodi/ushuru nafuu inayolipika kulingana na biashara zao.
Kukuza teknolojia na ubunifu, mambo yamebadirika ni muhimu kuwa na sera zinazohamasisha maendeleo ya teknolojia na ubunifu itasidia kuleta suluhisho la kisasa kwa changamoto mbalimbali za kiuchumi na kijamii, na kuongeza ushindani wa nchi kwenye soko la dunia na sio kila siku kuwa tegemezi wa teknolojia ya nchi zingine.
Kukuza utalii, kutumia rasilimali za asili na urithi wa kitamaduni zilizopo ili kukuza sekta ya utalii, ambayo inaweza kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya kigeni na ajira. Pia kufanya utalii unaovutia ikiwa sambamba na viingilio nafuu ili kuvutia zaidi watu wengi kuja kutembea Tanzania, kufanya matangazo katika viwanja vya ndege vya ndani na nje ya nchi.
Kuhamasisha kilimo cha biashara zaidi, kuboresha sekta ya elimu kwa kuhamasisha kilimo cha biashara, matumizi ya teknolojia kwenye kilimo cha kisasa, na kuongeza thamani kupitia usindikaji wa mazao. Hii itasaidia kuongeza mapato ya wakulima na kupunguza utegemezi wa kilimo cha kujikimu. Pia wakulima waruhusiwe kuuza mazao ya nje ya nchi na kazi ya serikali iwe kuwatafutia masoko imara ya mazao yao.
Kuvutia wawekezaji wa nje na ndani ya nchi, kutengeneza mazingira mazuri ya biashra ya kuvutia wawekezaji na kupunguza urasimu, kuhakikisha utulivu wa kisiasa na sera na kutoa vivutio kwa wawekezaji wa nje pia na wawekezaji wa ndani kuwatengenezea mazingira ya kuaminika zaidi ili wawekeze na kukuza uchumi.
Kuweka sheria za kupeana madaraka, kuongozwa na chama kimoja miaka 60 na changamoto bado zipo kibao, nadhani ni muda wa kuachiana madaraka na vyama vingine ili kutengeneza viongozi bora wanaofikiria mabadiriko na sio kila siku kuwa na chama kimoja, hii inapunguza ubunifu na uwajibikaji.
#TANZANIATUNAYOITAKA, #TANZANIATABASAMU

Upvote
2