Taifa lilipotekwa Nyara, Usalama wa Taifa walikuwa wapi?

Hivi , wadau Usalama wa Taifa bado upo?

Hicho kitu usalama wa Taifa hakipo kabisa Tanzania! Kwa mtazamo rahisi kabisa hawa walitakiwa kuwa watu wa kwanza kujua kuhusu lolote linalohatarisha usalama wa nchi, kiuchumi, kijamii na kwa namna yoyote. Walikuwa wapi wakati watu wanaiba tena kwa kufoji vielelezo, inawezekana deal zote hao jamaa ndio wanatumika kuzichonga. Madawa ya kulevya kila kona, tena watu wazito wanajihusisha nao, ufisadi ndio huo, bado tuamini tunaweza kulala tukiamini kuna usalama hapa? Ndio maana yule mshikaji akaamua hata aende Ikulu aibe ua, kwani nchi hii haina usalama wowote!!
 
Wana JF,

Mtoa hoja na`wote mliochangia hii mada nafikiri kuna kitu tunakisahau hapa. Kama alivyoeleza mwanakijiji hawa UWT wanapashwa wanuse habari na watoe taarifa kwa mkuu wa nchi na polisi kwa ajili ya kuingilia kati na kusimamisha uovu wowote ambao tayari unakuwa umepangwa. Sasa katika mazingira ambayo mkuu wa nchi kwa mfano na kwa ushahidi wa "marehemu Balali" wizi wa pesa za EPA ulikuwa na baraka za Mkapa mlitegemea UWT wafanye nini? Kama ufisadi wote unaofanyika nchi unamhusisha na mkuu wa nchi ambaye ndiye anapshwa awe mtekelezaji mkuu wa ushushushu wa UWT mnategemea kitu gani kitatokea? Je mmesahau story ya Kampuni ya Deep Green? Wanasema pesa zilibaki baada ya uchotaji zilipelekwa kwenye account ya usalama wa taifa. Sasa mlitarajia hawa wasaidie kuzuia ufisadi wakati nao ni`sehemu ya huo ufisadi?

Kama tunataka UWT ifanye kazi kama inavyotakiwa, basi tuhakikishe tuna mkuu wa nchi ambaye ni msafi na mzalendo mwenye uchungu nchi na umasikini walio nao wananchi. Lakini kama mkuu wa nchi atatoka kwa hawa wa chama cha mafisadi, tutawapigia kelele UWT lakini hata nao hawana pumzi kama juhudi zao hakuna wa kuziunga mkono.

Tiba
 
hivi kunaweza kuwa naabadiliko yaliyo kwisha kufanywa juu ya hii adara?
 
 
Jf ya zamani ilikuwa mubashara kabisa,yaan ni hoja juu ya hoja.

Sio hii yasasa iliyojaa kizazi chenye laana ns akili fupi..Et leo mange kimambi kawa think tanker wao!
 
Mmmaaa!! Mkuu toa msaada wa constructive ideal mfano nini kifanye?? Na nini kisifanyike kwa hao ndugu zetu, sasa twende wapi tukapate ushauri mwenzetu, ndugu yetuu,Mwl mwl Nyerere iiiiiih Taifa, ooo taifa pamoja twasema kwaheri Baba Mwl Nyerereee!!
 
Mmmaaa!! Mkuu toa msaada wa constructive ideal mfano nini kifanye?? Na nini kisifanyike kwa hao ndugu zetu, sasa twende wapi tukapate ushauri mwenzetu, ndugu yetuu,Mwl mwl Nyerere iiiiiih Taifa, ooo taifa pamoja twasema kwaheri Baba Mwl Nyerereee!!
 
Mzee Dr Hassy Kitine, Cornell Mwang'onda, Othman Rashid pumzikeni wazee wetu, mliitoa Tanzania mbali kwa usahihi kweli kweli ramani mliochora bado inasomeka haijafutika na haifutiki
 
Sasa hivi ndio hawa wanavamia vituo vya habari kina clouds media na plan za kuteka wabunge na kuwaua kama Bashe alivyosema leo

Ndio wamefikia hapa kama idara nyeti ya nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…