Taifa linawahitaji kina David Kufulila, Zitto Kabwe na John Mnyika wa kipindi kile

Taifa linawahitaji kina David Kufulila, Zitto Kabwe na John Mnyika wa kipindi kile

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
441
Reaction score
1,065
Kwa hakika mambo yakiendelea kwenda yanavyoenda ipo siku nchi itatawaliwa kwa asilimia mia moja na wakoloni usiniulize ni wakoloni wa aina gani kwani hata humu ndani wamo

Taifa limekosa vijana waibua hoja badala yake limepata vijana waibua vihoja (Kampeni za kufungia X)

Taifa limekosa watu wa kuhoji badala yake lina vijana waimba mapambio viongozi wanafanya walitakalo bila wasiwasi

Taifa limepungukiwa na watu wenye kusimamia ukweli badala yake linazalisha machawa

Walioshuhudia enzi za "ujana" wa kina Zito Kabwe, John Mnyika, David Kafulila, Mh. Mbowe, Tundu Lisu, Marehemu Mtikila, na wengine kadhaa watakubaliana na mimi kuwa kwasasa viongozi hawana watu wa kuwa challenge na pengine Mh. Rais Samia angeongoza kipindi kile tungeshuhudia Rais wa nchi akijiuzulu au kutoa machozi hadharani si kwa makosa yake ila ya watendaji wake wanaoshindwa kumshauri vizuri

Leo tunasikia mbuga za wananyama amepewa mwarabu hakuna hoja wala tetemeko bungeni kama ilivyowahi kutokea ya ESCROW

Bandari tunaambiwa imetoa gawio kubwa mwaka huu kwasabanu ya DP WORLD ambao hata hawajaanza ku opareti halafu "chawa" wanapiga makofi na hakuna wa kukemea na bungeni pako shwari?!

Vyuo vikuu karibu vyote vimekuwa matawi ya watawala kuanzia watoa mihadhara hadi wanoa bongo wote bongo zimelala

Nani wa kulikomboa Taifa?

Vijana Sekondari kwenye somo la historia kidato cha tatu wanasoma "establishment of colonialism" kwamba kuna viongozi wa kijadi waliingia mikataba ya ulaghai na mawakala wa ukoloni kwasababu hawakujua kilichoandikwa wala lengo la hao mawakala hatimaye wakafanikisha nchi kutawaliwa

Walimu wanakumbuka kuwaambia kuwa hayo mambo yanajirudia sasa tena kwa watu wanaojiita wasomi?

Zitto Kabwe, David Kafulila, Mh. Mbowe, Tundu Lisu na wengineo walifanya kazi yao kwa kipindi chao, enzi zao zimeisha na kama Taifa hatuna budi kuwashukuru kwa kazi waliyofanya. Hawa watu wanashindwa kukaa nje ya ulingo wa mapambano kwasababu pengine hawaoni mbadala wao.

Kwa hali iliyopo sasa nani wakuachiwa kijiti? Wasomi na elimu zao wamekubali kuwa machawa. Wasanii na vipaji vyao wamekubali kuwa machawa, vijana na nguvu zao wamekubali kuwa machawa.

Taifa linazalisha vijana wanaofurahi kuitwa "vijana wa hovyo na machawa" badala ya kuitwa majasiri. Kijana msomi anapokubali na kufurahia kuitwa majina mabaya kama chawa nani atalikomboa Taifa?

Nchi imeingia laana viongozi wa dini nao wamelala hakuna wa kukemea. Nani atalikomboa Taifa hili endapo mambo yasiyo sawa yanaonekana sawa machoni pa wasomi?
 
Kafulila kawapa kiasi gani? Na mimi anipe uchawa nauweza
Mkuu, hata kama sasa hivi ametulia anakula mema ya nchi na watawala "waovu" bado alifanya kazi yake vizuri kwa wakati wake.

Kuna wakati usipoeleweka inabidi ukae chini ule kinachokuja. Ndicho kilichotokea kwa Kafulila na Zito Kabwe na hivi karibuni Mbowe ataungana nao. Hii haimaanishi tusahau mchango wao, sisi wenyewe wananchi tumeshindwa kuwapa sapoti wao wafanyeje sasa
 
Washazeeka hao. Kuna vijana under 25 wako vizuri kichwani. Wekeni mifumo ya kisiasa vizuri wajitokeze ili waoneshe uwezo wao. Mnawataka hao wazee wa nn?
 
Washazeeka hao. Kuna vijana under 25 wako vizuri kichwani. Wekeni mifumo ya kisiasa vizuri wajitokeze ili waoneshe uwezo wao. Mnawataka hao wazee wa nn?
Hakuna aliyesema anawataka, soma mada vizuri acha uvivu. Hao under 25 ndio tunaowaongelea hatuwaoni? Wanasubiri mifumo ipi? Nyerere alisubiri wakoloni wamuwekee mfumo?
 
Wote ni wasaliti. Hakuna aliyelisaidia Taifa tusidanganyane.. wote wanafaidi kimtindo utajiri wa Tanganyika
 
Back
Top Bottom