Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Hili lipo wazi kabisa sasa hivi taifa letu wananchi wake wana hofu kubwa kwenye mioyo yao. Hofu juu ya ugonjwa wa Covid -19. Hasa baada ya kuwa na vifo vingi sana ndani ya siku nne zilizopita. Na hii sio imetokea hapa Tanzania tu hata nchi zilizoendelea kama Uk na Usa watu wana hofu.
Kwa mantiki hii wizara ya afya iwe na utaratibu wa kutoa tiba ya saikolojia kupitia vyombo vya habari Tv, Radio na Magazeti. Ili kuwaondolea wananchi hofu. Maana wananchi wengi wanadhani ukipata Covid-19 basi hauponi. Hata Usa nchi ambayo inaongoza kwa vifo takribani 55000+ waliopona ni wengi kuliko waliofariki sababu waliopona ni 250000+
Hivyo ni muhimu sana watu kujengwa kisaikolojia hasa kipindi hiki ambapo sababu ya hofu tu mtu analala na mask kitandani. Sababu ya hofu tu mtu anakuwa kama mtoto mdogo asipomuona mkuu wa nchi kwenye runinga anajua mambo ni magumu.
Maana amezoea akiona kwenye ziara zake akifika sehemu moto unawaka.Hivyo hofu inamjaa kuwa labda ugonjwa utaenea sana sababu mkuu wa nchi haonekani akienda Muhimbili au Mlongazila.
Hivyo naomba wizara kupita watalaamu wenu muanze kutoa hii tiba ya saikolojia ni muhimu sana kipindi hiki.