Taifa lolote ni zao la maadili hakuna taifa lolote litakalozaliwa na kuwa kubwa pasipo maadili

Taifa lolote ni zao la maadili hakuna taifa lolote litakalozaliwa na kuwa kubwa pasipo maadili

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Taifa lolote ni zao la maadili hakuna taifa lolote litakalozaliwa na kuwa kubwa pasipo maadili.

Viongozi ndio wanaotengeneza jamii, mawazo yao na maamuzi yao yana madhara makubwa kwa jamii husika. Ili jamii ipige hatua moja kuelekea nyingine inategemea sana akili na busara za viongozi. Aina ya viongozi jamii iliyonayo hutengeneza aina ya taifa.

Mtu mwenye akili hawezi kutegemea kiongozi mwovu ajenge jamii ya watu wema au kiongozi asiyetenda haki asimamie utawala wa haki na sheria. Mtu hutoa alichonacho katika hifadhi yake huwezi kutoa usichonacho.

Viongozi ndio wanaowajibika kwa mabadiliko yeyote katika nchi yawe mabaya au mazuri. Aina ya viongozi taifa ilionao hutengeneza aina ya jamii na taifa.

Mwelekeo wetu kama taifa utategemea sana akili , busara na hekima za viongozi wetu lakini pia maono yao. Taifa lisilo na maono ni taifa lililo gizani. Ni taifa ambalo halijui linapokwenda.

Hakuna taifa litakalo jengwa na kuendelea pasipo ''Ethics''.

Mataifa hulindwa kwa busara na hekima za viongozi na hubomolewa kwa ujinga wa watu katika mataifa hayo.

Hakuna maliasili yeyote itakayotusaidia kama hatutatengeneza watu wetu katika tabia zinazofaa. Ni watu wanaojenga mataifa na kuyekuza enyi ndugu zangu. Kuendelea kwa taifa hili kutategemea sana akili za watu wetu, nidhamu zao na utayari wao wa kuona taifa hili likinyanyuka.

Tunaweza kuwa na kila aina ya maliasili na ni kweli tumezungukwa nazo lakini bila utayari wa watu wetu kutaka kujiendeleza kama taifa hakuna kitakachofanyika.

Naamini tuna watu wana akili katika taifa hili ni wakati sasa wa kuacha ubinafsi na kuwa na malengo ya pamoja kama taifa. Mpaka lini sisi watu weusi tutaendeleza mgawanyiko miongoni mwetu badala ya kuwa wamoja? mpaka lini tutaendelea kukubali kutawaliwa?

Kunyanyuka na kuanguka kwa tawala yeyote ile, kunategemea sana misingi ya kimaadili na kinidhamu ya taifa hilo, pasipo nidhamu taifa lolote haliwezi kupiga hatua kimaendeleo, taifa lisilo kuwa na nidhamu ni kama mbegu zilizomwagwa shambani bila mpangilio mzuri haziwezi kuzalisha chochote. Ni muhimu sasa kujenga nidhamu na muelekeo katika taifa letu. Nidhamu huleta dira.

Hatutaweza kuendeleza taifa hili na kulikabidhi kwa kizazi kingine pasipo nidhamu na maadili. Viongozi wa kesho ni muhimu kujengwa sasa.

Kama tuna maliasili kibao katika ardhi yetu lakini maendeleo yetu ni hafifu ni lazima tujiulize uwezo wetu wa kiakili wa kutumia maliasili ili kubadili jamii zetu. Kama sio uwezo wetu wa kiakili basi tujiulize utayari wetu wa kuona jamii zetu zikibadilika na kupiga hatua katika maendeleo.

Lakini maendeleo haya sio ya vitu tu bali maendeleo ya kiakili ya watu wetu. Tungependa watu wetu wawe wenye akili wakue ili waweze kujenga taifa lao wenyewe na kuliheshimu. Tungependa kujenga mahusiano ya watu wetu na ufahamu wao juu ya utaifa.

Tutawezaje kujenga taifa hili bila nidhamu? nidhamu kwa viongozi, nidhamu kwa wananchi? bila kuheshimu taifa hili ambalo faida zote tunazipata humo kama raia ?

Tumekuwa wabinafsi kila mtu akiangalia nafsi yake kwa mtazamo huu tulio nao sasa kama taifa hatutafika mbali. Tunahitaji uongozi katika taifa hili ili kubadili muelekeo huu.

Mifumo ya kijamii imeparaganyika hakuna maono, kwa mwelekeo huu tulionao tusahau kuhusu Tanzania iliyokuwa ikiitwa kisiwa cha amani futeni katika akili zenu ni muda tu haujafika mtalia kama mataifa mengine yanavyolia kwa kukosa amani. Nchi huendeshwa kwa busara za viongozi, pale busara inapotoweka kuonyesha uongozi taifa huangamia.

Taifa ni umoja pasipo umoja hakuna taifa, kwa kiongozi yeyote yule makini na mwenye nia ya dhati kwa nchi yake, atafanya kila liwezekanalo ili watu wake wawe wamoja, kwakuwa pasipokuwa na umoja taifa lolote halitaweza kufikisha malengo yake.

Ni muhimu kutambua kwamba serikali haiwezi kujenga nchi peke yake pasipo jitihada za dhati na kujitolea kwa raia wanaojenga nchi hiyo, kiongozi mzuri ni yule mwenye uwezo wa ku organize na kuhamasisha watu wake katika kuleta maendeleo ya taifa lao wenyewe.




Ni muhimu kwa kiongozi yeyote yule kujenga uzalendo kwa watu wake, kuwafanya watu wake wajitambue kwanini wao ni Taifa na wana malengo gani kwa wao kuwa pamoja.

Lazima kuwe na kitu kinachowaunganisha pamoja, lazima kuwe na dira inayowaongoza kama watu walioamua kuishi pamoja, lazima wajue wanapotaka kuelekea. hii ni kazi ya kiongozi kuonyesha njia.

Lazima awe mtu mwenye kuaminiwa, mwenye hekima na busara za kutosha kuongoza watu, lazima watu wamuamini kutokana na matendo yake na maneno yake. Ni lazima awe na maono.

Kwahiyo ''ethics'' ni muhimu sana katika taifa, hakuna taifa litakaloweza kuendelea pasipo ethics. Hakuna taifa litakaloweza kuendelea pasipo kuwathamini watu wenye fikra bora.


Hakuna taifa litakaloweza kuendelea pasipo nidhamu kwa watu wake. Ili taifa liendelee ni lazima liache ujinga wake lifuate mambo yenye akili.


Taifa lolote ni zao la maadili hakuna taifa lolote litakalozaliwa na kuwa kubwa pasipo maadili. Hakuna taifa lolote litakalo zaliwa pasipo fikra na watu wake kuwa wenye kufikiri.


Pasipo nidhamu hakuna taifa lolote litakalojengeka. Kama tutapuuzia fikra na kufikiri tukafanya maamuzi kutokana na hisia zetu na tamaa zetu tusahau kuhusu maendeleo.

Kila mtu katika taifa hili ana wajibu tatu ambazo misingi yake pia ipo katika maadili; wajibu wake binafsi na kwa familia, wajibu kwa jamii na wajibu kwa taifa. Vitu hivi vitatu kama vikizingatiwa taifa letu litatoka hapa lilipo na kufika mbali sana.
 
Somo lako mkuu ni zuri sana, siku za nyuma niliwahi kujiuliza kwa kina sana hadi nikaanzisha thread hapa nikiwa nauliza swali hilo hilo kuwa Tanzania tulikosea wapi hadi tukafikia kuwa taifa lisilokuwa na maadili wala uzalendo? Miaka ya nyuma kulikuwa na uzalendo sana nchini kiasi kuwa hata wakati wa kwenda vitani uganda, kuna mgambo wengi sana waliopelekwa kule bila kuuliza malipo, yaani uzalendo wa kulitumikia taifa ulikuwa ni namba moja halafu rewards zinakuja baadaye. Leo hii taifa lote kila mtu anataka kuliraua kutokea mezani kwake. Imenishangaza kusikia kuwa Wizara ya serikali inadai kuwa mahesbau pungufu ya TRA ndiyo yatumiwe na bunge halafu yale mahesabu sahihi ya EWURA yapuuzwe; hili ni jambo la ajabu sana amabalo linatokana na taifa kukosa maadili hata kwa viongozi wakuu kama waziri na katibu mkuu wa wizara.
 
Mkuu Shayu naomba unielimishe. Mataifa yetu yalianzishwa na wakoloni. Je maadili gani yalitumika?
 
Wakoloni haqakuwa na lengo la kuanzisha Taifa bali Koloni ambalo watalinyonya na kuchujua resources kwa manufaa yao. Maadili kwao wao haikuwa priority.
 
Wakoloni haqakuwa na lengo la kuanzisha Taifa bali Koloni ambalo watalinyonya na kuchujua resources kwa manufaa yao. Maadili kwao wao haikuwa priority.

Shayu:

Kwa hiyo utakubaliana na mimi nikisema kuwa taifa kama Tanzania lilikuja kwa bahati nasibu. Walioanzisha walitaka koloni kwa manufaa yao. Na waliodahi uhuru waliungana sio kwa maana ya kuanzisha taifa lenye maadili, bali kumuondoa mkoloni (their common enemy).

Hivyo maadili unayoyazungumza kwa nchi kama Tanzania ni kitu kinachopatikana baada ya nchi kuwepo na watu kuona umuhimu wa maadili kwa manufaa yao.
 
Baada ya kuwaondoa wakoloni ilikuwa ni muhimu kuunda values na ethics za nchi kwa sababu bila vitu hivi sisi kama taifa hatutafika mbali.
 
Kujakwa bahati nasibu nakubaliana na wewe haiukuwa plan yetu.
 
Baada ya kuwaondoa wakoloni ilikuwa ni muhimu kuunda values na ethics za nchi kwa sababu bila vitu hivi sisi kama taifa hatutafika mbali.

Kujakwa bahati nasibu nakubaliana na wewe haiukuwa plan yetu.


Mara nyingi values na ethics zinakuja kutokana na matukio ya kihistoria. Sio vitu vya kupandikizwa. Tatizo kubwa vitu vingi venye malengo mazuri tuna-amrishwa na viongozi wa juu au mataifa yanayotoa misaada bila wananchi wa kawaida kuwa na historia navyo.

Kwa mfano katika miaka ya 80, vyombo vya usalama, sheria na utawala vilishindwa kuwapa huduma wanazostahili wakazi wa mikoa ya Shinyanga, Mwanza. Walipochoka walihamua kuanzisha vyombo vyao vya ulinzi "SunguSungu" zilivyokuwa na ufanisi mkubwa kuliko vyombo vya kiserikali.

Ukiangalia kwa undani muundo wa sungusungu ulikuwa na historia kwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Tabora. Labda wakazi wa mikoa hiyo wangekuwa na ufanisi mkubwa kama wangeruhusiwa kwa kiasa fulani kufanya vitu wanavyojua.
 
Values and ethics lazima zipandwe haziji zenyewe.
 
Back
Top Bottom