Tatizo la Tanzania si kocha. Ni wachezaji, wanaotokana na mfumo mbovu wa malezi ya kisoka tangu wakiwa watoto.Hii inafanya wasiwe na nidhamu ya soka,kujitambua na mambo mengi ya namna hiyo.Kwa hapa bongo hata akija Mourinho,Ferguson, ama Wenger mambo yatakuwa kama yalivy😵mbi langu kwa serikali kupitia wizara husika.Ijaribu kutoa scholarship ya soka kwa watoto (chini ya miaka 17) wanaotokana na mashindano ya cocacola kila mwaka, wakasome katika academy za soka ulaya.Naamini tutafikia mafanikio tunayoyataka.Na hili linawezekana, utaratibu huu ukiendelea kwa michezo yote, TZ tutashinda katika michezo yote ikiwa ni pamoja na ile ya Olympic.Scholarships hizi ziwafikie pia makocha vijana na wachezaji wa zamani kama akina Chambua,Pawasa,Edibily baadaye waje wachukue mikoba ya kufundisha timu za Taifa.