samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Inasemekana timu ya taifa ya tanzania haijawahi kuibuka na ushindi ikiwa inashuhudiwa na rais kikwete kama mtazamaji au mgeni rasmi na kwamba mara zote hizo imekua ikiambulia kichapo au sare. Naomba mwenye kumbukumbu sahihi anijuze.
Anamikosi na kisa, ni jinsi anavyowatesa watanzania na alivyolayimisha kuongoza ilhali anajua hana ana akili hiyo.
Tuliishinda 2-1 bukina faso nae akiwepo uwanjani. Nyingine zote akiwepo ni kipigo au sare.
Kama hali ndo hiyo inabidi TFF wabadili upepo waanze kumualika mtoto wa mkulima pinda au shein inawezekana hao wakawa na nyota ya USHINDI ,
Ni zaidi ya kuwa na roho ngumu......kweli ana roho ngumu sana kukubali kila siku kuja uwanjani na kutoka akiwa ameinamisha kichwa chini, mi nisingeweza uhuni huu lazima wote wanaohusika wangekuwa wanapata mshikemshike mpaka watarekebisha kila kona kwenye game next time. Nchi masikini kama hii inabidi kuiendesha bila kuonyesha sura ya tabasamu kwa kila mtu, kuna section inabidi unakuwa mkali mpaka watu wanakuwa hawalali kuhakikisha mambo yanaenda sawa , ukiweka pressure kwa viongozi then hao viongozi wakaiweka hiyo pressure kwa makocha then kwa wachezaji lazima kitaeleweka tu.
Yaani haya maneno alayopewa Jakaya yangekuwa ni sumu angeshakuwa amekufa siku nyingi ila waswahili huwa wanasema "mtasema mchana usiku mtalala" "kelel za chura..........." "dua ya mwewe..........." ninamuonea sana huruma JK