Taifa Stars: Hivi Kocha wa "Conditioning" wa timu yetu ni Nani?

Taifa Stars: Hivi Kocha wa "Conditioning" wa timu yetu ni Nani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Timu zote za kisasa na zenye uwezo wa kushindana kwenye mashindano ya kimataifa zinakuwa na Conditioning Coach. Huyu ni kocha msaidizi wa Kocha Mkuu katika eneo la "Conditioning". Conditioning kimsingi ni kuhakikisha kuwa wachezaji na timu nzima inakuwa katika fikra sahihi za kiakili zinapokaribiana na mechi yoyote. Baada ya kufungwa mechi ya kwanza na Senegal niligundua mara moja kuwa kuna tatizo kubwa sana la conditioning.

Wanaonifahamu wanajua kuwa mimi nilicheza soka shule ya Sekondari (kuanzia form 1 hadi form six) nikiwa wakati mwingine kama kocha mchezaji. Nilicheza nafasi ya mlinda mlango maarufu enzi kama "Nyanda". Hivyo, nina mapenzi na ushabiki mkubwa wa soka. Nina uhakika siko peke yangu kati ya wazee kama mimi ambao tunapenda soka kwa sababu tulilipenda toka utotoni na kama soka enzi zetu lingekuwa ni la kulipa labda tungefukuzia ajira kwenye kabumbu.

Turudi baada ya kufungwa; wachezaji wetu mara moja walianza kuzungumza na kusema "tulicheza na timu kubwa".. "wachezaji wao wanacheza Ulaya"... n.k nilipoona hili na hata baada ya mechi ya Algeria na comeback ya Kenya nilijua kuwa tuna tatizo kubwa sana la kufikiri na kisaikolojia. Tunajisahau tunacheza na binadamu wenzetu kama sisi ambao nao wakipigwa chenga wanahungaika na wakivishwa kanzu wanajisikia hasira kama vile wakipigwa tobo!

Bila ya shaka kuna misingi mikubwa zaidi ya matatizo ya timu zetu (siyo Taifa Stars tu). Na kubwa kama wengi ambavyo wameshalidokeza ni "maandalizi". Hili la maandalizi labda nina mtazamo kama wa baadhi ya watu humu kwamba ni zaidi ya "mechi za maandalizi" au motisha n.k. ZInahusiana na mfumo mzima wa soka kuanzia ngazi za chini kabisa. Na siyo tu katika soka bali pia katika michezo mingine.

Hata hivyo, hata ukiwa na hayo mengine yote ni lazima uwe na wachezaji wanaofikiri sawasawa na ambao wako katika afya nzuri ya mwili (fit). Ni jukumu la kocha huyu akisaidiana na daktari wa timu kuweza kuangalia maslahi ya wachezaji kiafya ya akili na mwili.

Naomba nitoe mifano ya timu kubwa na sehemu ya makocha wao wa "maandalizi ya kiakili" yaani conditioning coaches.

Mike Clegg- alikuwa Strength and Conditioning Coach wa MANU (2000-2011) chini ya Alex Ferguson
Andreas Kornmayer - Kocha wa "fitness and conditioning" wa Liverpool
Darcy Norman - kocha wa "movement and conditioning" wa Timu ya Taifa ya Wanaume ya Marekani
Nick Shedd - kocha wa "strength and conditioning" wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Marekani

Hii ni mifano tu michache. Turudi kwenye swali letu...

Anayemsaidia Amulike kwenye mambo ya conditioning ni nani?
 
Conditioning ilikua safi kabisa kimwili na kiakili
 

Attachments

  • VID-20190702-WA0024.mp4
    5.4 MB
Back
Top Bottom