Taifa Stars hiyoo AFCON, hakuna timu ya kutuzuia!

Moshi25

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,555
Reaction score
4,118
Kwanza kabisa niseme wazi timu yetu ya taifa ni nzuri na inaupiga mwingi sana sio kibonde tena huko tushatoka.

Ukiangalia mechi za Taifa Stars na Congo DR huwa hazina mnyonge. Lolote humkuta yoyote, hapo rank za FIFA huwa hazina kazi , bampa to bampa, piga nami nikupige, Congo DR mabishoo , mapro hawataki kuumia, tukiwakazia na kuwaparamia maungoni, huwa tunatoka bila madhara makubwa, maana hawataki kuguswa!

Mechi ya mwisho ya Afcon kule Ivory Coast, Taifa Stars ilizembea tu sababu ilikuwa na uwezo wa kushinda hasa baada ya mpango wa kuzuia kufanikiwa na Congo DR kuchoka kushambulia, nawakumbusha tu DRC ni timu imetuacha mbali kisoka, kule Ivory Coast, tuliingia kuzuia hadi Congo DR wakapoteana badala ya kufunga sasa eti tukaridhika na droo na kupigiana pasi nyingi za kijinga jinga ili kupoteza muda.

Ukweli binafsi nilimaindi sana maana droo ilikuwa inaturudisha home sasa sikujua kipi kiliwafurahisha hawa wachezaji wetu. Nafasi ya kufunga ilikuwepo wao wakachagua droo, mechi ile ya mwisho kwenye makundi hatukuwa na cha kupoteza ni bora Taifa Stars wangefunguka na kupambana ikibidi hata wafungwe kuliko walivyofanya kutafuta droo kwa nguvu, droo isiyo na faida!!

Soma Pia, Full Time Tanzania 1 - 0 Guinea | 2025 AFCON Qualifier | Estadio Benjamin Mkapa | 19.11.2024

Binafsi nilitafsiri ni ushamba wa wachezaji wetu kushangilia droo ambayo nayo ni kushindwa tu!! Ujinga mtupu. Taifa Stars walikuwa hopeless kabisa that match day!

Mechi zetu zijazo na Congo DR hasa keshokutwa mbinu iwe ile ile kukaba kwa nguvu timu nzima kwa dkk 30 za mwanzo kila kipindi na kuwaparamia maungoni, tukikaba bila kuchoka hatufungwi, wale jamaa wametuzidi uwezo kisoka sasa ni lazima tucheze nao ule mpira wa vurugu wa kina Yondani na Nyoso na Akaminko na kisha tunashambulia kwa kasi dkk 15 za mwisho kila kipindi tukiwa makini kutumia chances tutakazopata, naamini tutashinda.

Ni vizuri tufanye mazoezi ya kukimbia sana tuwe na pumzi kukimbia na kukaba bila kuchoka kwa dkk tisini, bila kukaba sana tutapigwa nyingi, tukimbie sana na hapo hapo tukitegemea counter attack ambayo ndiyo silaha yetu kubwa.

Mabeki acheni sifa za kijinga na kuzubaa zubaa na kukaa na mipira, kazi iwe moja tu kuanua mbele. Kosa moja la mabeki na Guinea likazaa goli moja jepesi sana, Baka kesha clear, mpira unazagaa, Nondo kazubaa kabaki kutoa macho badala ya kuanua, goli la kizembe sana, ile haipaswi kujirudia.

Beki ya Taifa Stars isaidiane maana ndiyo mhimili wa timu kwa sasa.

Halafu Mkude mbona haitwi Stars na anakiwasha Yanga? Kuna yule mido wa Azam mechi ya Zambia alipwaya sana, alipoingia tulishambuliwa sana nusu uwanja, ni muda tu ulituokoa ilikuwa tufungwe, yule hana uwezo kama Mkude.

Mkude aitwe tafadhali mechi zijazo ataimarisha sana katikati ambako ni dhaifu sana kwasasa kwa maoni yangu.

Samatta needs to prove his quality, atuoneshe yeye ni mchezaji ghali zaidi, si lazima afunge but ile kazi yake nzuri ya amsha amsha, jamani twendeni mbele tukasake goli huwa ina madhara makubwa kwa wapinzani.

Kibu Denis anapoichezea Taifa Stars huwa wa moto sana, kijana anakaba mwanzo mwisho, anakimbia sana na kuwa mchezaji pekee mwenye msaada mkubwa zaidi uwanjani kwa kupunguza mashambulizi ya wapinzani.

Mudathir ndie injini ya Stars kwasasa ila bado ana shida ya kucheza marafu yake ya kijinga , huko DRC rafu hazifai atapigwa red card, awe makini, but huyu Mudathir anapaswa kucheza dkk tisini kuzuia madhara na masifa ya kina Mayele. Mudathir hapaswi kukaa benchi.

Saaduni ni bonge la mchezaji, anakiwasha sana Azam. sasa ni zamu yake huko Congo DR kutuonesha uwezo wake mkubwa alionao. Mechi za Congo DR ndo za ku-shine kijana aache uoga ajiamini piga wakongo goli mbili safi kila mechi, yeye na Mzize walazimishe kupasua ngome ndani ya penati box ya Congo DR kusababisha penati hata mbili.

Feitoto sasa ameanza kuonesha makali yake Taifa Stars, hapaswi kuendelea kuleta ujuaji na mbwembwe zake za kujidai kuzunguka na mpira, mbwembwe zisizo na faida, Feitoto anapaswa kukua na kuacha kucheza kwa kutafuta sifa, anapaswa kuongeza umakini na kufunga kila mechi ya timu yake ya Taifa kwa mashuti ya nje ya box.

Kutinga Afcon mapema inawezekana kabisa, hapa inatakiwa tu tuwapige Congo DR kama ngoma, tuwafunge nje, ndani, kisha bila huruma tunawakanda Guinea tatu bila wakija kwa Mkapa na kumaliza kazi nzuri kwa kuifumua kibonde Ethiopia kwao, mbili bila majibu. Uwezo tunao.

Otherwise all the best for my Tanzanian natioal team.

Binafsi naamini uwezo wa kushinda mechi zote upo , soka letu limekua, vijana wajivunie taifa lao wapambane kufia uwanjani washinde huko kama kawaida yao ya kushinda mechi za ugenini. Wakiukosa ushindi basi hata droo ipatikane si mbaya.
 
Ivi huaga unaagalia game za team yetu ya taifa au unatupanga? Maana mimi nimeshudia ile gamena Ethiopia niliona vituko kweli kweli
 
Kwanza kabisa niseme wazi timu yetu ya taifa ni nzuri na inaupiga mwingi sana sio kibonde tena huko tushatoka.

Ukiangalia mechi za Taifa Stars na Congo DR huwa hazina mnyonge. Lolote humkuta yoyote, hapo rank za FIFA huwa hazina kazi , bampa to bampa, piga nami nikupige, Congo DR mabishoo , mapro hawataki kuumia, tukiwakazia na kuwaparamia maungoni, huwa tunatoka bila madhara makubwa, maana hawataki kuguswa!

Mechi ya mwisho ya Afcon kule Ivory Coast, Taifa Stars ilizembea tu sababu ilikuwa na uwezo wa kushinda hasa baada ya mpango wa kuzuia kufanikiwa na Congo DR kuchoka kushambulia, nawakumbusha tu DRC ni timu imetuacha mbali kisoka, kule Ivory Coast, tuliingia kuzuia hadi Congo DR wakapoteana badala ya kufunga sasa eti tukaridhika na droo na kupigiana pasi nyingi za kijinga jinga ili kupoteza muda, ukweli binafsi nilimaindi sana maana droo ilikuwa inaturudisha home sasa sikujua kipi kiliwafurahisha hawa wachezaji wetu. Nafasi ya kufunga ilikuwepo wao wakachagua droo, mechi ile ya mwisho kwenye makundi hatukuwa na cha kupoteza ni bora Taifa Stars wangefunguka na kupambana ikibidi hata wafungwe kuliko walivyofanya kutafuta droo kwa nguvu, droo isiyo na faida!! Binafsi nilitafsiri ni ushamba wa wachezaji wetu kushangilia droo ambayo nayo ni kushindwa tu!! Ujinga mtupu. Taifa Stars walikuwa hopeless kabisa that match day!

Mechi zetu zijazo na Congo DR hasa keshokutwa mbinu iwe ile ile kukaba kwa nguvu timu nzima kwa dkk 30 za mwanzo kila kipindi na kuwaparamia maungoni, tukikaba bila kuchoka hatufungwi, wale jamaa wametuzidi uwezo kisoka sasa ni lazima tucheze nao ule mpira wa vurugu wa kina Yondani na Nyoso na Akaminko na kisha tunashambulia kwa kasi dkk 15 za mwisho kila kipindi tukiwa makini kutumia chances tutakazopata, naamini tutashinda.

Ni vizuri tufanye mazoezi ya kukimbia sana tuwe na pumzi kukimbia na kukaba bila kuchoka kwa dkk tisini, bila kukaba sana tutapigwa nyingi, tukimbie sana na hapo hapo tukitegemea counter attack ambayo ndiyo silaha yetu kubwa.

Mabeki acheni sifa za kijinga na kuzubaa zubaa na kukaa na mipira, kazi iwe moja tu kuanua mbele. Kosa moja la mabeki na Guinea likazaa goli moja jepesi sana, Baka kesha clear, mpira unazagaa, Nondo kazubaa kabaki kutoa macho badala ya kuanua, goli la kizembe sana, ile haipaswi kujirudia. Beki ya Taifa Stars isaidiane maana ndiyo mhimili wa timu kwa sasa.

Halafu Mkude mbona haitwi Stars na anakiwasha Yanga? Kuna yule mido wa Azam mechi ya Zambia alipwaya sana, alipoingia tulishambuliwa sana nusu uwanja, ni muda tu ulituokoa ilikuwa tufungwe, yule hana uwezo kama Mkude. Mkude aitwe tafadhali mechi zijazo ataimarisha sana katikati ambako ni dhaifu sana kwasasa kwa maoni yangu.

Samatta needs to prove his quality, atuoneshe yeye ni mchezaji ghali zaidi, si lazima afunge but ile kazi yake nzuri ya amsha amsha, jamani twendeni mbele tukasake goli huwa ina madhara makubwa kwa wapinzani.

Kibu Denis anapoichezea Taifa Stars huwa wa moto sana, kijana anakaba mwanzo mwisho, anakimbia sana na kuwa mchezaji pekee mwenye msaada mkubwa zaidi uwanjani kwa kupunguza mashambulizi ya wapinzani.

Mudathir ndie injini ya Stars kwasasa ila bado ana shida ya kucheza marafu yake ya kijinga , huko DRC rafu hazifai atapigwa red card, awe makini, but huyu Mudathir anapaswa kucheza dkk tisini kuzuia madhara na masifa ya kina Mayele. Mudathir hapaswi kukaa benchi.

Saaduni ni bonge la mchezaji, anakiwasha sana Azam. sasa ni zamu yake huko Congo DR kutuonesha uwezo wake mkubwa alionao. Mechi za Congo DR ndo za ku-shine kijana aache uoga ajiamini piga wakongo goli mbili safi kila mechi, yeye na Mzize walazimishe kupasua ngome ndani ya penati box ya Congo DR kusababisha penati hata mbili.

Feitoto sasa ameanza kuonesha makali yake Taifa Stars, hapaswi kuendelea kuleta ujuaji na mbwembwe zake za kujidai kuzunguka na mpira, mbwembwe zisizo na faida, Feitoto anapaswa kukua na kuacha kucheza kwa kutafuta sifa, anapaswa kuongeza umakini na kufunga kila mechi ya timu yake ya Taifa kwa mashuti ya nje ya box.

Kutinga Afcon mapema inawezekana kabisa, hapa inatakiwa tu tuwapige Congo DR kama ngoma, tuwafunge nje, ndani, kisha bila huruma tunawakanda Guinea tatu bila wakija kwa Mkapa na kumaliza kazi nzuri kwa kuifumua kibonde Ethiopia kwao, mbili bila majibu. Uwezo tunao.

Otherwise all the best for my Tanzanian natioal team.

Binafsi naamini uwezo wa kushinda mechi zote upo , soka letu limekua, vijana wajivunie taifa lao wapambane kufia uwanjani washinde huko kama kawaida yao ya kushinda mechi za ugenini. Wakiukosa ushindi basi hata droo ipatikane si mbaya.
Kocha mle hamna.
 
Hivi kwanini Salum Abubakar aka Sure boy haitwi timu ya taifa? Naona kama angefanya vzr pale kati na Mudathiri Yahya...
 
Back
Top Bottom