TAIFA STARS IMEPIGANA KWA KIWANGO CHAKE TUSIIBEZE SABABU:

TAIFA STARS IMEPIGANA KWA KIWANGO CHAKE TUSIIBEZE SABABU:

Somi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2009
Posts
3,921
Reaction score
4,858
1. Tuliingia afcon baada ya kushika nafasi ya pili chupuchupu tukose nafasi , mpaka katimu kama lesotho kalitufunga shauri ya maandalizi duni na programu dhaifu ya tff

2.Wachezaji bado hawajapata uzoefu wa kutosha kwenye mashindano makubwa na kucheza ligi kubwa ikiwamo stamina ,technique
Yule mfungaji wa Kenya anacheza girona ya la liga,
Senegal na algeria wote ulaya

3.Ratiba ya ligi ya tff ni mbovu hakuna muda wa mapumziko kwa wachezaji.

4.Pengo la Morris lillishindwa kuzibika.

5.Timu haikukaa kambini muda wa kutosha na kutengeneza maelewano, wakati ligi ya Tanzania inaendelea Kenya walikuwa kambini ufaransa ( ingawa nao sioni wakiwa na nafasi ya kwenda raundi ya pili)

6.Timu haikupata mechi za majaribio ya kutosha .
7. Tff haijafanya kazi yoyote kuwatafuta na kuwashawishi wanasoka waliokuwa ulaya wenye asili ya Tanzania ambao tumekuwa tukiwasoma mara kwa mara wakitamani kuchezea tanzania, nchi za afrika magharibi wanafanya hivyo.
8. Vilabu vikubwa havikuzi wachezaji wazawa wenye vipaji Vinategemea wachezaji wa nje
9.Timu ilicheza kwa presha na Woga Sababu ilikuwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kushiriki afcon.
10. Tff haikuwa na mkakati wa ushindi kama kipindi cha kocha akiwa Marcio Maximo.
 
Hiyo number 7.CCM wanaogopa sana uraia pacha (dual citizenship) hivyo usitegemee kuwa mtu atakubali kuutupa uraia wake wa EU ili achezee stars.Hizo nchi za Africa magharibi unazosema wachezaji wake wana uraia wa nchi za ulaya na nchi zao za asili.
 
9.Timu ilicheza kwa presha na Woga Sababu ilikuwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kushiriki afcon.

Kuanzia Viongozi wa TFF, wa Timu ya Taifa a.k.a CCM stars na wachezaji wote ni watu tofauti na wale wa mwaka 1980, sasa presha wanaitoa wapi??

Kama wao ndio waliluwepo enzi hinzo wangeweza kupata presha kipindi hiki.

Hongereni Harambee Stars
 
TURUDI KWENYE HESABU ZETU

‘Hivi tukimfunga Algeria goli 5 bila, Kenya nae akatoa sare na Zambia ………… kisha Senegal akafungwa na Uganda, hapo tumuombee Misri apoteze, kisha Congo amfunge Sudan goli 3 bila.

Halafu game ya Nigeria na Ghana itoke sare ya bila kufungana

Si tutaingia robo fainali????

NEVER GIVEUP BWANA…………………

Muniwache bado nimevurugwa na matokeo ya jana
 
Sasa unasema tusiibeze imepambana kwa kiwango chake, timu imeshapoteza mechi mbili mfululizo, na tunategemea kupoteza tena mechi ya tatu, mweeeh kiwango gani tena hicho..?

Yaani ukishahusisha kitu chochote na sisiemu basi ujue ni failure..
 
Hiyo number 7.CCM wanaogopa sana uraia pacha (dual citizenship) hivyo usitegemee kuwa mtu atakubali kuutupa uraia wake wa EU ili achezee stars.Hizo nchi za Africa magharibi unazosema wachezaji wake wana uraia wa nchi za ulaya na nchi zao za asili.
Hio sio taifa stars Bali ni timu ya ccm full stop kwa hio wanaotakiwa kuhuzunika ni ccm wenyewe wengine tuachane nao.
 
Back
Top Bottom