Taifa Stars inaenda Cameroon 2019 , Uganda anakufa taifa March 2019

Malick M. Malick

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Posts
658
Reaction score
312
Nina matumaini makubwa sana wa Timu ya Taifa kushinda mchezo wa Uganda na kwenda Cameroon 2019

Timu Yetu ya Taifa imekua na tabia moja ikishinda mchezo mmoja, mara nyingi mechi inayofuata wanafanya vibaya Bila kujali mchezo huo unachezwa wapi
Nakumbuka kipindi cha Maximo tuliifunga Bukinafaso kwao goli moja, ikawa imebaki mechi moja nyumbani ili tuweze kufuzu kama best looser

Watanzania na timu tulijiandaa sana na tulilewa sifa sana baada ya kuifunga Bukinafaso kwao, tukawa tunacheza na Msumbiji Taifa

Dakika ya mwanzo tukafungwa goli na Tikotiko la mapema, goli halikurudi na safari ikaishia hapo.

Taifa Stars imeshawai kuifunga Tunisia 3 Katika uwanja wa Taifa, ila mechi iliyofuata tukafanya vibaya..

Mechi ya jana na Lethoto ilifika sehemu wachezaji wetu wakazoea mchezo wakawa hawakabi tena Mfano lile goli tulilofungwa watu walijaa golini Bila kutimiza majukumu yao

Mwisho tukafungwa goli rahisi wachezaji watambue wanatakiwa kuwa makini dakika zote tisini sio kuzoea mchezo, Timu za kiafrica zina hili tatizo.

TIMU YA TAIFA INAFUZU KWENDA CAMEROON, ila tukifika huko Cameroon tusipokua makini tutapata Tabu sana

Hivi inawezekanaje Madagascar na Mauritania wanafuzu Alafu sisi tushindwe, vijana wetu lazima wajitume
 
Mkuu bila ya kumuanzisha mkude, boco, kichuya, nyoni, yondani, manula, msuva game ya uganda tunapigwa vibaya sana.
.
Nimepata fursa ya kuhudhuria semina za mwl. Kashasha pale taifa mwaka 2017 ninauelewa mpira barabara sisi mpira hatuuwezi kabisa amini usiamini.
.
Bila kuwahonga millions of dollars uganda au kuwapa miradi ya maendeleo watatutia aibu ya karne.
 

Sasa kwakuwa mmenichokoza nawawekeeni hapa hapa na matokeo rasmi ya mechi ya Taifa Stars dhidi ya Uganda Cranes na Cape Verde dhidi ya Lesotho na nani atapita kati ya Tanzania, Lesotho na Cape Verde. Na hii ni kwa mujibu wa huyu huyu ' Mtaalam ' wangu hatari wa Kipemba.

Taarifa ikufikie popote pale ulipo ewe Mtanzania kwamba hiyo mechi yetu ya Uganda tutatoka sare ambayo itakuwa ama ya Magoli au isiyo na Magoli ila ni Sare ( Draw ) na mechi kati ya Cape Verde na Lesotho ni kwamba Cape Verde atashinda hivyo Kufikisha alama zake Saba ( 7 ) na kutuacha Tanzania na alama zetu Sita ( 6 ) na Lesotho watabaki na alama zao Tano ( 5 ) na hatimaye Cape Verde ndiyo ataungana rasmi na Uganda kwenda huko AFCON 2019.

Naomba hii ' post ' itunzwe na kila Mtu awe nayo kwani ndiyo ukweli wenyewe na hata Tanzania tufanye nini au tujitahidi kufanya juhudi zozote matokeo ndiyo hayo hayatabadilika. Ushauri wangu tu kwa TFF, Watanzania na hata Rais wetu Dkt. JPM ni kwamba hivi sasa tuwekeze nguvu zetu nyingi kwa Timu za Taifa za Vijana Serengeti Boys na Ngorongoro Heroes ili zifanye vyema katika michuano yao inayoshiriki sasa na pia tuanze sasa Kuiandaa Timu ya Taifa Stars ya Kufuzu na Kucheza AFCON ya 2021 ila hii ya Cameroon mwakani tumeshatepeta kama siyo kutokota na endeleeni tu Kudanganyana na Kupeana moyo.

Nimemaliza.
 
Mtani wangu hii kitu nilishawaambia wadau hapa jukwaani ,kabla ya mechi na Lesotho wakati wewe ukija na utabiri wako wa mtaalamu babu kwamba tutashinda Mimi nilikua nkiwataarifu kwamba Lesotho atatunyoa na droo tutatoa na UG alafu cape Verde atampiga Lesotho.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…