Taifa Stars/Kilimanjaro Stars tuifanyeje?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Taifa Stars imesukumwa nje ya mashindano ya awali ya kombe la dunia kwa aibu ya kipigo cha mabao 7-0 toka kwa Algeria. Kilimanjaro Stars (ya Tanzania Bara) imetupwa nje ya michuano ya Challenge kwa kutolewa na Ethiopia kwa penati. Hata Zanzibar Heroes nayo imetupwa nje.

Tuifanyaje Taifa Stars/Kilimanjaro Stars ili iweze kufanya vyema kwenye michuano ya kimataifa? Tuivunje na kuunda mpya? Tuiache na kuiimarisha iliyopo? Tufanyaje hasa? Inauma sana kushangilia timu za taifa za nje na kuiacha yetu ikidorora.

Tuchangie waungwana.

Nakala kwa Jamal Malinzi
 
Laana inaiandama timu ya taifa
 


#WhatWouldMagufuliDo?
 
...kila mtu aanze kulia pale alipo, km mama lishe lia kwenye banda lako, mwanafunzi; lia darasani, mwalimu; lia ofisini, nesi;lia wodini, wagonjwa lia wodini, Magufuli; lia ikulu, konda;lia mlangoni.... tulie ki kweli kweli kwa wiki moja,Mungu atatuhurumia!
 
Mbona ndio ipo hvyo cos kule zanzbar heros wanatoka haji mwinyi,canavaro,mudathir,mwadin wanakuja tia nguvu huku taifa starz,hata iyo kili statz wachezaj waliongezeka ni kessy,mkude tu so timu ni ile ile issue kwenye upangaji wa kocha inapofikia mechi ya taifa starz but timu ni ile ile tu na tofauti huku kili kaongezeka kwenye bench la ufundi mkinda na manyika senior
 
Vunja timu nzima. Tujitoe kabisa katika mashindano yoyote. Tukuze vijana u12-13 tuwasambaze kwenye academy tofauti duniani after 4 yrs tushiriki u17 then miaka 2 au 3 baadae hiyo ndo taifa stars. Hiyo ndio formula ya mpira no shortcut
 
Waziri mkuu mh. Majaliwa Kassim Majaliwa ni kocha tena anayetambulika na TFF, tumpe hizi timu, zitanyooka tu maana kasi yake nae si masihara!
 
Vunja timu nzima. Tujitoe kabisa katika mashindano yoyote. Tukuze vijana u12-13 tuwasambaze kwenye academy tofauti duniani after 4 yrs tushiriki u17 then miaka 2 au 3 baadae hiyo ndo taifa stars. Hiyo ndio formula ya mpira no shortcut
Mkuu,umenifanya nikose cha kuchangia kwa haraka kwani umeiba pointi zangu
thumb up mkuu!
 
...nasema hakuna kuvunja timu,tuendelee kushiriki mpk mwisho wa dunia!
 
Kwa Taifa stars inatakiwa turudi uwekezaji katika soka la vijana,Mashindano ya Copa Coca Cola,Airtel Rising Star yanazalisha wachezaji vijana watunze kwa kupelekwa katika academies ili baadae waje kuisaidia timu ya Taifa.Upande mwingine ni wa makocha bado hatupo vizuri sana,ni kweli tunataka makocha wazawa lakini uwezo na uzoefu wao ni mdogo katika mashindano ya kimataifa hasa kwakiwango cha timu ya taifa.Mfano Taifa stars iliyofungwa na Algeria mkurugenzi wa ufundi Kibadeni,Kocha mkuu mkwasa,Kili stars Kocha mkuu kibadeni mkurugenzi wa ufundi Mkwasa je Tanzania hatuna makocha wengine?Tunachanganya na mambo ya kujuana katika kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…