Taifa Stars kufungwa imeniuma sana

msumeno

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2009
Posts
2,826
Reaction score
1,734
Niko njiani narudi kazini,, tuko mwendo wa kawaida tu jioni saa kumi na mbili ya hapa, tunasikiliza BBC.

Mara mtangazaji anasema Kocha mpya wa timu ya Tanzania Mkwasa ateua timu mpya... kwa unyonge nikasema '' aaa sisi kila siku kufungwa tu'' yeye huku akicheka akasema ''Tanzania mtaweza mangapi?? mengine lazima mshindwe.... ndo hapo nilipo muuliza ni yepi tumeweza sasa??!!..... bila kumug'unya maneno akasema.

Barabara zote kuu mmejenga... sasa tukinunua gari au kuleta gari toka DAR inafika bado mpya kabisa maana ni gudro tu toka DSM mpaka Gisenyi.

Lakini pia Jeshi lenu ni imara na lenye weledi sana... tumeshuhudia hapa ( hapo nikawa sina la kusema maana sikuwepo kipindi kile)

Demokrasia yenu iko wazi na ni mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine, hapo nikasema kweli kabisa

Asante M-congo ila kufungwa kwa Taifa stars naumia sana aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…