Nimekuwa nikifuatilia michezo ya kombe la COSAFA inayoendelea mpaka sasa katika nchi ya Africa Kusini hasa kwenye michezo ambayo timu yetu imekuwa ikicheza.Mungu jalia timu yetu imeweza kufurukuta mpaka kufikia hatua ya nusu fainali japo kwa mbinde na hii imetokana na wapinzani wetu tunaokutana nao hawakuwa wamejiandaa vya kutosha. Nisiwe mnafiki nianze kwa kuwapongeza wachezaji wetu kwa kufikia hatua ya nusu fainali kwani hakuna mtu alitarajia hilo achilia mbali waandaaji wa Mashindano waliotualika kama wageni "wachovu".Nasema wachovu kwa kuwa pamoja na kualikwa ilibidi tupitie mchakato wa kucheza na timu vibonde ili kuweza kufauru hatua ya robo fainali na kuweza kukutana na timu kama Africa Kusini ambazo wao walikuwa mapumzikoni wakisubiri vibonde wa kwenye makundi tutoane.Tuyaache hayo pamoja na kufanikiwa kufika hatua ya nusu fainali,timu yetu imeonyesha kiwango kibovu kupita kiasi pengine cha chini kuliko hata timu tulizozifunga kama Africa Kusini...Malawi...hata Leshotho tunaocheza nao sasa hivi kutafuta mshindi wa tatu (Dk.86 live SS4) kitu iliyopelelea kutufanya wapenzi wa soka kupata presha dk.90 zoote tokea mpira unaanza mpaka mwisho...yafuatayo ni mapungufu niliyoyaona na kama hayajafanyiwa kazi basi tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu mpaka atakaporudi Yesu.1.Wachezaji wetu karibia woote (98%) hawaelewi nini wanatakiwa kufanya uwanjani..hakuna malengo,wachezaji wanapapara mtu akipewaa pasi anaanza kutetemeka kabla ya kupokea mpira by the time unamfikia either utamngonga au atatoa pasi butu,stamina ni tatizo kubwa (stamina sio lazima kuwa na mwili mkubwa nieleweke) tatizo kwetu mtu akifanikiwa kupiga chenga ya kwanza kinachofuata ni kuanguka na mpira mwenyewe (Msuva, Kichuya) na wengine wengi,mbaya zaidi walimu nao wamekariri kikosi hakuna improvement...wala hakuna strategy mpira unaavyoanza mpaka kuisha ni purukushani dk zoote,Kukimbizana mpaka mpira unaisha....Kati ya mambo yaloniumiza saana pamooja na timu kuwa mbovu ni kuona wachezaji ambao wamekuwa wakisifiwa kwenye ligi ya Vodacom kwa matarumbeta (Kichuya na msuva) wakionyesha kiwango cha chini kabisa kuanzia katika umiliki wa mpira,kufanya maamuzi (papara nyingi) kutoa pasi bila malengo. N.k...nikajiuliza hivi ndio hawa tunaowasikiaga wamazifunga yanga na Simba?..Kwa ufupi hali ni mbaya saana kupita kiasi yaani kama ningekuwa napaewa nafasi ya kuchagua timu kwa hawa wa sasa atleaast ningewabakiza Maguri,Mkami (kapteni),Yasini, Erasto ,Nyoni, beki number tatu sijui sudi au said