Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,072
September 3 2016 ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilicheza mchezo wake wa mwisho wa kuwania kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2017 na timu taifa ya Nigeria katika uwanja wa Uyo uliopo katika jimbo la Akwa Ibom State. Katika mchezo huo, Taifa Stars walifungwa goli 1-0.
Licha ya kufungwa, Taifa Stars walionesha uwezo mkubwa kimchezo kiasi cha gavana wa jimbo hilo kuwapa zawadi ya dola 10000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 21. Fedha hizo walipewa katika hafla ya chakula cha pamoja baada ya mchezo huo.
Sasa nauliza, kama thamani ya vijana wetu imeonekana huko ughaibuni, sisi kama taifa tunaituzaje? Au ndio nabii hakubaliki kwao?