Ni mambo ya ajabu hivi unafikiri Tanzania katika miaka ya karibuni watafikia angalau kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa no rafiki yangu usijidanganye soka la Tanzania halipandi kwa sababu nyingi mno. mpaka hapo wabongo watakapokaa chini na kuzifanyia kazi sababu moja baada ya nyingine ndipo tataanza kuona raha ya mchezo wa mpira wa miguu,. Nataka nikupe baadhi ya sababu kwanza viongozi wa vilabu wengi wameomba uongozi kuganga njaa au kujipatia kipato. kwa hali hiyo jitihada kubwa na mtazamo ni fedha.yuko tayari kuhonga wachezaji ili timu yake ishindwe iwe sababu ya mtu kuingia madarakani. Pili maandalizi ya timu zetu ni hafifu mno tunaandaa timu bado wiki mbili za mashindano kwa hali hiyo huwezi kuwashinda wachezaji ambao wako kambini mwaka mzima. Tatu serikali haijatoa kipaumbele katika michezo wanaona ni kupoteza muda. Nne wachezaji wetu wanachukuliwa wakiwa wameshakomaa na baadhi wanavuta bangi, zaidi ya hayo ni wachovu na wananjaa kali wananunulika kirahisi ninaweze kuandika kutwa nzima. Wakati nchi hii ilikuwa ianfanya vizuri katika tasnia hii ya michezo watanzania walikuwa wanaipenda nchi yao walicheza kwa moyo wa uzalendo sio kwa fedha. nafikiri inatakiwa moyo wa uzalendo usiishie kwenye masuala ya kisiasa iwe mpaka kwenye michezo. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.