Taifa Stars mpya: Dida, Nyoni, Munishi out. Barthez, Manyika, Kibadeni ndani!

Taifa Stars mpya: Dida, Nyoni, Munishi out. Barthez, Manyika, Kibadeni ndani!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
KdsBe2


KOCHA mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha timu hiyo pia akimteua gwiji Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden' kuwa Mshauri wake wa Ufundi.

Mkwasa ameteuliwa jana kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, akirithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij aliyefukuzwa mwishoni mwa wiki kufuataia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza kufuzu michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Rwanda.

Na leo Mkwasa ameteua wachezaji 26 watakaoingia kambini Jumamosi kuanza maandalizi ya kwenda kupindua kipigo cha 3-0 wiki mbili zijazo mjini Kampala, Uganda ili kusonga mbele CHAN.

Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari leo. Kulia ni Msaidizi wake, Hemed Morocco.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam, Mkwasa amesema kwamba amemteua pia Manyika Peter kuwa kocha wa makipa.

Amesema benchi lake la Ufundi linakamilishwa na Mtunza Vifaa, Hussein Swedi ‘Gaga', Meneja Juma Mgunda na Mratibu Msafiri Mgoyi, wakati Daktari atatajwa baadaye.

Mkwasa ametaja kikosi kipya cha Taifa Stars akimtema aliyekuwa kipa namba moja chini ya Nooij, Deo Munishi ‘Dida', akiwachukua makipa watatu; Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ali (Azam FC) na Ally Mustafa ‘Barthez' (Yanga).

Mabeki ni Shomary Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohammed Hussein ‘Tshabalala' (Simba SC), Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM), Nadir Haroub ‘Cannavaro' (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC), Hassan Isihaka Simba SC, Aggrey Morris (Azam FC).

Viungo ni Jonas Mkude (Simba SC), Abdi Banda (Simba SC), Salum Telelea (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Ramadhani Singano ‘Messi' Simba SC na Deus Kaseke (Yanga).

Washambuliaji ni Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Ame Ali (Mtibwa Sugar), wakati wengine ambao wamewekwa akiba ni Juma Abdul wa Yanga SC, Mudathir Yahya wa Azam FC na Samuel Kamuntu wa JKT Ruvu.

Kesho, benchi la Ufundi la Stars litakutana na wachezaji wote walioteuliwa katika hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam kuwaelimisha juu ya uzalendo na Mkwasa amesema Jumamosi timu itaenda kuweka kambi nje ya mji.

Chanzo: BinZubeiry Blog

 

Attachments

  • MKWASA.jpg
    MKWASA.jpg
    55.1 KB · Views: 490
Kila la kheri Master.Charles Boniface Mkwasa tunaipenda timu yetu ila mfumo mzima wa soka letu unatuangusha nakuomba utufute machungu aliyotuachia mtalii NOOIJ sijui no ni nini huku aende zake amekuja kutuletea rekodi ya Aibu sana
 
Bado striker wa kati hatuna
 
Tunakutakia safari nje katika kuirejesha stars kwenye mstari.
 
Afadhali, Master Mkwasa ameleta sura ngeni kama Barthez, Michael Aidan, Ame Ali na Atupele Green.. hawa naimani watawapush sana wale waliokua wakidhani namba za taifa stars ni hatimiliki zao. Naimani siku zijazo, sura ngeni zitaongezeka zaidi.
 
Hamna kitu, naye atatolewa kama huyo aliyefukuzwa. Ukiwachuka "mataahira", for that matter unteachables , ukawaweka shule huwezi kumlaumu mwalimu, nadhani nimeeleweka. let us wait and see! Mpira sio kama maigizo ya wema and the like!
 
[TABLE="width: 431"]
[TR]
[TD]Mwadini Ally-[/TD]
[TD]azam[/TD]
[TD="align: right"]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Shomari Kapombe-Azam
[/TD]
[TD]azam[/TD]
[TD="align: right"]2[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Aggrey Morris-Azam
[/TD]
[TD]azam[/TD]
[TD="align: right"]3[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Frank Domayo-Azam
[/TD]
[TD]azam[/TD]
[TD="align: right"]4[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ame Ally-Azam
[/TD]
[TD]azam[/TD]
[TD="align: right"]5[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Atupele Green-Kagera Sugar
[/TD]
[TD]kagera[/TD]
[TD="align: right"]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mudathir Khamis-KMKM
[/TD]
[TD]kmkm[/TD]
[TD="align: right"]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mwinyi Hajj-KMKM
[/TD]
[TD]kmkm[/TD]
[TD="align: right"]2[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Rashid Mandawa-Mwadui
[/TD]
[TD]mwadui[/TD]
[TD="align: right"]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Michael Haidan-Ruvu Shooting
[/TD]
[TD]ruvu[/TD]
[TD="align: right"]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mohammed Hussein-Simba
[/TD]
[TD]simba[/TD]
[TD="align: right"]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Hassan Isihaka-Simba
[/TD]
[TD]simba[/TD]
[TD="align: right"]2[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Jonas Mkude-Simba
[/TD]
[TD]simba[/TD]
[TD="align: right"]3[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Abdi Banda-Simba
[/TD]
[TD]simba[/TD]
[TD="align: right"]4[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Said Ndemla-Simba
[/TD]
[TD]simba[/TD]
[TD="align: right"]5[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ramadhan Singano-Simba
[/TD]
[TD]simba[/TD]
[TD="align: right"]6[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ally Mustapha-Yanga
[/TD]
[TD]Yang[/TD]
[TD="align: right"]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Nadir Haroub-Yanga
[/TD]
[TD]Yang[/TD]
[TD="align: right"]2[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kelvin Yondani-Yanga
[/TD]
[TD]Yang[/TD]
[TD="align: right"]3[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Simon Msuva-Yanga
[/TD]
[TD]Yang[/TD]
[TD="align: right"]4[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Salum Telela-Yanga
[/TD]
[TD]Yang[/TD]
[TD="align: right"]5[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Deus Kaseke-Yanga
[/TD]
[TD]Yang[/TD]
[TD="align: right"]6[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Tutajie tungemchukua nan hapo

Sina wa kupropose ila namaanisha kwa ujumla kama taifa hatuna striker mkali, yaani ni tatizo la kitaifa siyo kwamba nasema wamechagua vibaya
 
[table="width: 431"]
[tr]
[td]mwadini ally-[/td]
[td]azam[/td]
[td="align: Right"]1[/td]
[/tr]
[tr]
[td]shomari kapombe-azam[/td]
[td]azam[/td]
[td="align: Right"]2[/td]
[/tr]
[tr]
[td]aggrey morris-azam[/td]
[td]azam[/td]
[td="align: Right"]3[/td]
[/tr]
[tr]
[td]frank domayo-azam[/td]
[td]azam[/td]
[td="align: Right"]4[/td]
[/tr]
[tr]
[td]ame ally-azam[/td]
[td]azam[/td]
[td="align: Right"]5[/td]
[/tr]
[tr]
[td]atupele green-kagera sugar[/td]
[td]kagera[/td]
[td="align: Right"]1[/td]
[/tr]
[tr]
[td]mudathir khamis-kmkm[/td]
[td]kmkm[/td]
[td="align: Right"]1[/td]
[/tr]
[tr]
[td]mwinyi hajj-kmkm[/td]
[td]kmkm[/td]
[td="align: Right"]2[/td]
[/tr]
[tr]
[td]rashid mandawa-mwadui[/td]
[td]mwadui[/td]
[td="align: Right"]1[/td]
[/tr]
[tr]
[td]michael haidan-ruvu shooting[/td]
[td]ruvu[/td]
[td="align: Right"]1[/td]
[/tr]
[tr]
[td]mohammed hussein-simba[/td]
[td]simba[/td]
[td="align: Right"]1[/td]
[/tr]
[tr]
[td]hassan isihaka-simba[/td]
[td]simba[/td]
[td="align: Right"]2[/td]
[/tr]
[tr]
[td]jonas mkude-simba[/td]
[td]simba[/td]
[td="align: Right"]3[/td]
[/tr]
[tr]
[td]abdi banda-simba[/td]
[td]simba[/td]
[td="align: Right"]4[/td]
[/tr]
[tr]
[td]said ndemla-simba[/td]
[td]simba[/td]
[td="align: Right"]5[/td]
[/tr]
[tr]
[td]ramadhan singano-simba[/td]
[td]simba[/td]
[td="align: Right"]6[/td]
[/tr]
[tr]
[td]ally mustapha-yanga[/td]
[td]yang[/td]
[td="align: Right"]1[/td]
[/tr]
[tr]
[td]nadir haroub-yanga[/td]
[td]yang[/td]
[td="align: Right"]2[/td]
[/tr]
[tr]
[td]kelvin yondani-yanga[/td]
[td]yang[/td]
[td="align: Right"]3[/td]
[/tr]
[tr]
[td]simon msuva-yanga[/td]
[td]yang[/td]
[td="align: Right"]4[/td]
[/tr]
[tr]
[td]salum telela-yanga[/td]
[td]yang[/td]
[td="align: Right"]5[/td]
[/tr]
[tr]
[td]deus kaseke-yanga[/td]
[td]yang[/td]
[td="align: Right"]6[/td]
[/tr]
[/table]

kwa kuweka hili jedwali unamaanisha nini mkuu?....hivi canavaro bado hajioni na kujitathmini yeye mwenyewe kuwa sasa umri umemtupa mkono ajiondoe timu ya taifa kwa heshima?..na mwenzake yondani.
Pia huyu messi si hana timu huyu...kwanini umemuweka simba wakati tff walisema mkataba wake na simba ni batili...

Kwa sasa niishie hapo.
 
Tutabadilisha makocha,tutabadilisha wachezaji,kipigo kiko pale pale,bila mfumo madhubuti kwa wachezaji wa umri mdogo tutaendelea kuraumu tu.!!
 
Sina wa kupropose ila namaanisha kwa ujumla kama taifa hatuna striker mkali, yaani ni tatizo la kitaifa siyo kwamba nasema wamechagua vibaya
Ok ni kwel lakin tatizo tz si wachezaji tu km weng wanavosema tatizo hakuna wa kuvihamasisha hv vipaji vika maximise their effort km mpenz wa mpira utazijua timu km atletico Madrid ya simeone, Porto ya mourinho , Manchester ya sir Alex ( baadhi ya misimu) , sevila ya unai emery, hawakuwa NA wachezaji tishio ila walikuwa wanajua kuvitumia vipaji vya wachezaji kwa mda husika. Sikubalian na wachezaji hawafundishiki tatizo ni kwamba hatujapata kocha NA benchi la ufund ambalo linajua kuvitumia vipaji husika kwa mda husika
 
Back
Top Bottom