Taifa Stars na Seregenti Boys

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Jina la Taifa Stars lilibuniwa nadhani mwaka 1967 hivi wakati wa mashindano ya pili ya East African Senior Challenge Cup. Kabla ya hapo timu ya taifa ilikuwa ikijulikana kama Tanganyika National Team, na baada ya muungano ikajulikana kama Tanzania National Team.

Baada ya kuingia kwenye mashindano ya kimataifa ya under 20, timu ya Tanzania ilipewa jina la Serengeti Boys.

Kwa maoni yangu, naweza kuwa nakosea, jina la "Serengeti Boys" linaitangaza Tanzania kwa uwazi zaidi ya jina la "Taifa Stars."

Kuna haja ya kufanya mjadala kubadili jina la Taifa Stars kuwa jina jingine ambalo linakuwa linatangaza taifa kwa uwazi zaidi.

Matumizi ya neno la kiingereza "Stars" nayo yanaleta mushkeli kidogo kwa timu ambayo haijawahi kushinda mashindano makubwa ya kimataifa.
 
Tufanye yote kwa pamoja.
Mpira wetu ungekuwa mzuri hilo lingekuwa lishafanyika siku nyingi sana.

Tukipata mafanikio mengine yatafuata kwa urahisi sana

Tungejitutumu kama Venezuela kufika robo fainali ila tushaharibu na hatuna uwezekano tena wa kucheza mechi zaidi ya 3.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…