Taifa stars njia nyeupe AFCON 2019 kazi ni kwetu

Nemesis

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2008
Posts
5,517
Reaction score
4,477
Uganda the cranes wamefuza fainali zijazo za AFCON kwa kuifunga Cape Verde 1:0.

Hivyo Cape Verde wanabakia na point 4 na endapo wataifunga Lesotho mechi yao ya mwisho watafikisha point 7.

Taifa stars ikishinda kesho itakuwa na point 8 ambazo Cape Verde hawezi kuzifikia. Matokeo yakiwa tofauti tutalazimika kupambana kwa mbinde na Uganda mwakani ili kufuzu. Hata hivyo Uganda wapo vizuri sana, tupambane kiume kesho. Vijana wetu wafanye kweli.

Hongera Uganda, Tukaze daluga Taifa stars. Tunaweza kukumbusha historia ya mwaka 1980.

Msimamo ulivyo sasa
1. Uganda. 13
2. Taifa stars 5
3. Cape Verde. 4
4. Lesotho 2
 
hili group ni Uganda vs vibonde.
 
hili group ni Uganda vs vibonde.
Mkuu stars haijafungwa na Uganda. Tumecheza nao mechi moja kule kwao na iliisha kwa sare. Tunawasubiri Dar. Stars ndiyo timu pekee kwenye group ambayo haijafungwa na Uganda.
 
tz ya JPM haiwezi shinda kitu,tena ni bora watoke mapema kuliko kuja kutupa aibu huko mbeleni
Nafikiri hupo sahihi, kuna maisha nje ya siasa. Kila kitu kisijumuishwe kwenye siasa. Kuna nchi zina utawala mbaya ajabu, vita kila siku lakini michezo wapo vizuri. Hawa jirani zetu wenyewe wanae M7. Michezo isiingizwe kwenye siasa
 
Kichwa cha mwendawazimu
Aliwazalo mjinga ndilo humtokea. Ukiwaza ni kichwa cha mwendawazimu unakuwa hivyo hivyo na unajiandaa kunyolewa. Ukijiona mshindi unafanya jitihada za kushinda.
 
Itakuwa hivi wakuu wangu, Taifa stars atakufa kwa Lesotho afu droo na Uganda, Cape Verde atampiga Lesotho na kusonga mbele na point 7 ova! Samahani kwa niliowakwaza ila ukweli ndiyo huo
 
Njia nyeupe!!!!!!!!!!!!!!!!! inamaana wanaenda kcheza na vilema wasio na miguu ni wao wenye miguu peke yao?
 
Itakuwa hivi wakuu wangu, Taifa stars atakufa kwa Lesotho afu droo na Uganda, Cape Verde atampiga Lesotho na kusonga mbele na point 7 ova! Samahani kwa niliowakwaza ila ukweli ndiyo huo
Ni utabiri tu
 
Njia nyeupe!!!!!!!!!!!!!!!!! inamaana wanaenda kcheza na vilema wasio na miguu ni wao wenye miguu peke yao?
Nyeupe kwasababu Uganda ameshinda Leo. Cape Verde wangeshinda tungekuwa na njia ya Gizani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…