Comrade Ally Maftah
Member
- Nov 6, 2016
- 77
- 271
UCHAMBUZI WA Comrade Ally Maftah PACOME WA MCHONGO) Tanzania VS Guinea.
Katika viwango vya FIFA vinaonyesha Guinea ipo katika nafasi ya 77 na Tanzania tukiwa nafasi ya 113.
Mechi hii imechezewa Ivory Coast ikiwa Guinea ndio wenyeji wa mchezo huo, kwa sababu Guinea hawana kiwanja kinachokidhi viwango vya CAF kucheza mchezo huo wakati huo Tanzania tunavyo viwanja tumpongeze Dr Samia Suluhu Hasan kwa hatua hiyo, Ivory Coast ipo kusini mashariki mwa Guinea.
Katika kipindi cha kwanza ambapo tulimaliza dakika 45 tukiwa suluhu, Tanzania tulionekana kuzidiwa kidogo katika mchezo ambapo tulikuwa katika viwango vya chini vya mchezo 49% kwa Tanzania na 51 kwa Guinea huku tukiwa imara katika safu ya ulinzi na kupwaya kidogo kwenye ushambuliaji tukiwa hatuna kona hata moja, mashuti golini na tukiwa na kadi za njano 2.
Katika kipindi cha kwanza tulifanya mabadiliko baada ya Dikson Job kupata maumivu na kuingia Bakari Nondo Mwamnyeto.
Kipindi cha pili kinaaza huku Taifa stars ikiwajia Juu Guinea katika ushambuliaji lakini kwa bahati mbaya tunapigwa goli moja na Mohamed Bayo katika mazingira ambayo Ibrahim Baka alimkabili mshambuliaji huyo na kukosa usaidizi kutika kwa mabeki wa Tanzania kilichopelekea Mohamed Bayo kuupokonya mpira aliyopokonywa na Ibrahim Baka na kuupiga pembezoni mwa Ally Salum na kushindwa kuunyakua Dakika ya 57 tukawa tumelowa goli moja.
Feisal salum alifanya mashambulizi ya kupiga pasi ambayo haikukaa sawa kwenye miguu ya Balua,
Dakika ya 62 Feisal Salum alikongota mpira wa mbali na kitikisa nyavu za Guinea na kusawazisha Goli, tukawa na sare ya goli moja kwa moja
Mabadiliko yaliyofanywa na mwalimu kumtoa Balua na kumuingiza Paschal Msindo, na Waziri Juma na kumuingiza Himidi Mau yameuchangamsha mchezo
Dakika ya 89 Mudathiri anakutana na mpira uliotemwa na kipa wa Guinea ambao ulipigwa na Feisal Salum, na kuingiza nyavuni na kufanya Tanzania tuwe mbele kwa Goli moja ikiwa ni matokeo ya 2 kwa 1.
NYOTA WAMEMALIZA MCHEZO KWA USHINDI WA GOLI 2 KWA 1.
DRC CONGO NAFASI YA KWANZA AKIWA NA POINT 6 KATIKA KUNDI NA TANZANIA YA PILI AKIWA NA POINT 4.
Pia soma
- News Alert: - FT: Guinea 1-2 Taifa Stars | Kufuzu AFCON 2025 | Septemba 10, 2024| Charles Konan Banny Stadium