Taifa Stars, Robo Fainali na Dona - World Cup 2022

Taifa Stars, Robo Fainali na Dona - World Cup 2022

Dr Ahmed Albah-Shahwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2022
Posts
848
Reaction score
1,604
Wataalam,

Niipongeze Taifa Stars kushiriki na kuonyesha uzalendo na ushindani katika michuano ya kombe la dunia ingawa kuna mapungufu mawili matatu yanayosahihishika ni hatua kubwa kwa timu na serikali kwa ujumla tunajua huu ni mwanzo wa maendeleo mapana yajayo, tuizungumzie timu yetu;

Hali halisi - Tunakwama wapi?

Timu inajengwa kuanzia beki/nyuma


Ili ubebe kombe lolote hasa hasa kombe la dunia inabidi uwe na uwezo wa kuhimili vigingi, walau vya timu zote zinazoshiriki kwenye michuano ya kombe mahususi asilimia 50% ya ushindi wa mechi yoyote ile ni energy/mperampera/mbilingembilinge/intensity/morali/mori/mzuka kama wa beki wa zamani wa taifa Nsajigwa "Fuso" inayotumika kuzuia. Timu zote zinazo chukua kombe la dunia zinakuwa na wachezaji wa aina ya Fuso, Kuna ile Man U ya babu Fergie ilikuwa na kina Nemanja Vidic na Rio Ferdinand au aliekuwa anabaguliwa Patrice Evra wa Ufaransa, Pep Gadiola wa Man 6 alikuwa na kina Dejong yaani kiatu kibaki mpira uende au mpira ubaki kiatu kiende, 1998 Ufaransa wanabeba kombe la dunia walikuwa na kina Patrick Viera na Emanuel Petit, 2002 Brazil wanabeba kombe la dunia walikuwa na Cafu, 2006 Italy walikuwa na Canavaro(achana na huyu wa Utopolo mla urojo isingekuwa urojo angeipeleka utopolo AFCON maanake anajua) na Gatuso zamani Paolo Mardin, 2018 Ufaransa walikuwa na Ngolo Kante 2014 Spain alikuwa na Sergio Ramos, Puyol na Pique mme wake Shakira yaani hawa machizi soka lazima uwenao tu tofauti na hapo sahau! (Hao jamaa niliowataja hapo juu kama huna taarifa wamedata wanakaba hadi Kivuli)

Kiukweli ulinzi wa goli bado tuko nyuma sana ukiachilia mbali ujuzi wetu duni katika kukaba(marking) kuna swala la afya hili nitaliongelea kiupana baadae.
Dimbani, wachezaji wakishaachwa na foward/mshambuliaji wa timu pinzani hawana nguvu ya kumkimbiza iliwalau wampige kikumbo/push au wakabie kutokea mbele matokeo yake kila red kadi tuliopata kati ya 4 ni ya kosa hili hili moja poor marking/ukabaji dhaifu unakuta beki anakaba akitokea nyuma hana mbio ya kumbiza adui mwisho anamkanyaga mchezaji direct/moja kwa moja mguuni bila kuugusa mpira au unakuta mabeki wote wamejikusanya sehemu moja inapelekea kuwapa Japan nafasi ya kumpima kipa kuna magoli zaidi ya 4 tumefungwa ni yakumpima kipa yote katika yote kipa na washambuliaji wanajua ila beki bado.

Kipindi cha kina Wayne Rooney wa Manchester United aliitwa Mrisho Ngasa kwenda kuichezea hiyo timu ya Uingereza wataalamu wa timu wakaalikwa walivomcheki tu Ngasa wakagundua anautapia mlo wakamshauri aanze kula vizuri wakamtolea mfano Rooney unaambiwa jamaa anauwezo wa kula mbuzi peke yake kama breakfast sasa ilivokuja kwa Ngasa hakuweza kula paja timu ikamshinda akarudi bongo kuja kuichezea Mbeya City yaani kaacha hela mezani kisa tu utapia mlo ambao angeweza kuutokomeza laiti TFF wasingeingiza siasa uchawara kwenye soka nakulea vijana kiroho safi, vijana watunzwe kuanzia miaka nane TFF iache uhuni ianzishe academy za kuibua vipaji iliwanaojua waondolewe huo utapia mlo tunajua haiwezi kuondoa kwa watanzania wote.

Ukimfuatilia Hashim Thabit utagundua hili swala la lishe aliwahi kukutana nalo alivyofika US alikuwa anatakiwa kula vyuku vya kutosha, mwenyewe akakiri kwamba angerudi bongo baada ya kuzoea zile menyu angekufa njaa hii yote kwa nini? michezo ya Kikapu na Mpira inatumia nguvu kwanza akili baadae uweze kukimbizana na maadui kwanza tactics/mbinu tutajifunza baadae.

Dimbani, kuna ile hali inamwingia mchezaji akiicheki njemba inayoondoka na mpira ilivoshiba anakata tamaa laiti na wao wangekuwa na afya, walau wangekimbizana, wachezaji inabidi wapate mshauri wa saikolojia maana wameshaathirika wanaweza wasipone wasipozingatiwa. Sio kwa ile morari waliokuwa nayo wa Japan na Colombia jamaa walikuwa wameshiba. Kama Taifa pia tunadhalilika inaonekana tuna njaa kulinganisha na mataifa mengine ilhali misosi iko kibao na tunauzia majirani.

Wenzetu wanafanyaje

Mfano Almando Diego Maradona au Pele mwenyewe king of soccer huyu jamaa alikuwa kajazia kweli na mpira hautoki kizembe mguuni kwake na huu ulikuwa ule mpira mkubwa wa zamani achana na jabulani hizi za 2010 kuendelea au Pele babake Ayew wa Ufaransa anaechezea Ghana huyu nae alikuwa mtu kweli kashiba yaani hadi uutoe mpira mguuni kwake utasimulia. 1994 Cameroon inatolewa nusu fainali ilikuwa na njemba kama kina Roger miller.
Kuna ile nigeria ya kina Babayaro, Babangida, JJ Okacha na Nwanko Kanu hawajamaa walikuwa wameshiba
Afu kuna ile cameroon ya kina Samweli Etoo ya miaka ya 2010 walikuwa wanavaa vijezi vyao vya kubana kinoma unakuta mchezaji mbavu hasa.

2010 Ghana wanatupeleka robo fainali wanatolewa kwa zengwe na Uruguay walikuwa na ulinzi wa kutosha kina Stephen Appia midfielders walikuwa kina Michael Essien washambuliaji walikuwa Asamoah Gyan hawa jamaa walikuwa wamekula dona. Basi tu kiwewe Gyan kwenye penati ya ushindi kagongesha posti ya juu.

Kuna huyu cheupe wa Buyern Munich na Senegal eehee Sadio Mane huyu jamaa kashiba kinoma ndio maana anauwezo wa kuhimili mikiki ya mabeki wa Ujerumani bundasliga yaani abaki mtu mpira uende au aende mtu mpira ubaki

Delima, Drogba unakuta njemba zimeshiba hatari yaani hadi umwangushe Didier Drogba kwenye box au Delima R9 inabidi utumie crane na ukimdondosha ujue penati vile vile Messi watu wanamchukulia poa lakini hadi Messi adondoke ujue kuna dona imetumika hawanguki kizembe wakiwa karibu na goli.

Kuna Gaucho yaani jamaa alikuwa njemba haanguki kizembe. Wadau wanahakikisha mchezaji kashiba, kuna ule mtindo wake kucheza anakuwekea upaja au anakupa mwili tu hivi uhangaike nao mpira anapiga danadana kifupi anaufanya atakavyo wakati wewe unahangaika na paja uko.

Mwisho, hata hii timu ya Nigeria iliyotolewa na Colombia unakuta wachezaji wameshiba vizuri tu wana miili hatari hata ukilinganisha nguvu yao wanayotumia kukaba na timu yetu ya Taifa kunatofauti kubwa sana yaani(mbingu na ardhi) wanapaki fuso wanapanda na wanashuka wote ndio sababu ya penati penati "penat shoot outs" zote alizopata Naijeria, kwa lugha nyingine Naijeria wana uwezo sawa tu na Columbia kwa sababu penati hazina mwenyewe sio timu zetu wachezaji afya ya kuungaunga afu sisi ni Dona Cantri.

Sasa sisi tufanyeje.
Serikali iache siasa kwenye mambo ya msingi kama kuchukua kombe la dunia iige wenzetu Ghana wa 2010. Yaani mbunge anajiwakilisha mwenyewe anapewa milioni 16 kwa mwezi inaacha kutenga hata laki tano kwa ajili ya msosi wa madogo wa kwenye academy watakao wakilisha nchi kwenye kombe la dunia, uzuri zikianzishwa academy za watoto kuanzia miaka nane hata kupata wafadhili ni rahisi achilia mbali serikali watu wanahela mbele huko hawajui wazielekeze wapi.

Mwalimu achague mabeki wenye urefu wakuridhisha hata wanne TFF ihakikishe fungu la maaana linaelekezwa kwenye mazoezi ya gym na misosi.

Ule mpera mpera tuliopelekwa na Columbia na Japan ni lishe tu ndio iliyotuangusha Japan hawana ujuzi mkubwa sana kuliko sisi katika tactics/mikakati. Hawa jamaa wana falsafa moja inayoitwa Kaizen maana yake maboresho endelevu hado hado kwa mfano kama unataka kuwa bingwa wa kupiga push ups hata 100, leo unaanza na pushup 10 kuanzia kesho utakuwa ukiongeza push up 1 yaani leo 10 kesho 11 kesho kutwa 12 nakuendelea timu zetu inabidi ziichukue hii kama zinataka kweli kubeba kombe la dunia yaani lengo linatakiwa liwe mchezaji awe na mwili kama wa CR7 yaani uwiano/ratio wa misuli na kimo viendane awepo kocha wa gym anaezingatia msosi na chuma (mwalimu wa tactic/mipango anajua). Wachezaji iwe marufuku kutumia kama vyakula energy drink, viepe, k vant, kuvuta bange, kupiga puli na kuendekeza mademu etc. Natabiri tusipo punguza ngono na gambe mademu watachukua kombe la dunia kabla yetu.


Tanzania sio kichwa cha mwendawezimu kama wahuni wanavyosema ili kukwepa majukumu yao husika Simbasc na Taifa Stars ni ushahidi tosha.

#kataawahunidawasconatanesco
 
Sehemu kubwa ya vitu umeandika ni story za vijiweni...

Eti Rooney alikuwa ana uwezo wa kula mbuzi mzima kama sehemu ya breakfast, kwani umeambiwa ni pro wrestler huyo?
 
Sehemu kubwa ya vitu umeandika ni story za vijiweni...

Eti Rooney alikuwa ana uwezo wa kula mbuzi mzima kama sehemu ya breakfast, kwani umeambiwa ni pro wrestler huyo?
Mkuu wenzetu wanazingatia sana kula nisababu pia wanamaumbo makubwa huwez kuta mtu kala kiepe akaenda kulala haiwezekani
 
Amini usiamini kuna watanzania wanaweza kula mbuzi mzima na si mbuzi pekee yake hata na nguna pembeni kama liko mtoa mada ni aina ya hao watanzania huyu ni mwingine achilia mbali wale wa mjengoni kwa Tulia pia wana huu uwezo mcheki huyu jamaa kuna picha nlikuwa nayo ya Rooney ntakuletea alikuwa anapata breakfast unaweza kumcheck huyu mwamba anaitwa Saidi Msosi.
 
Back
Top Bottom