Taifa Stars Vs Malawi

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
2,092
Reaction score
2,123
Mechi inatarajiwa kuanza saa 16:00 itarushwa live kupitia supersport 7 na ZBC, kikosi kitakachoanza dhidi ya Malawi leo
1.Ally mustapha 'barthez'
2.Shomari Kapombe
3.Haji Mwinyi
4.Kelvin Yondani
5.Nadir Haroub 'Cannavaro'
6.Himid Mao
7.Mrisho Ngassa
8.Said Ndemla
9.Mbwana Samatta
10.Thomas Ulimwengu
11.Farid Mussa

Kila la kheri Taifa Stars'
==============

Mechi imeanza na hadi sasa Tanzania inaongoza goli 2 dhidi ya Malawi yaliyofungwa na Samatta na Thomas Ulimwengu. Mechi hii ni hatua ya mwanzo kuelekea kufuzu kombe la dunia nchini Urusi 2018.

:A S soccer:Mbwana Samata
:A S soccer:Thomas Ulimwengu

45' Mpira ni mapumziko

Mpira umerejea na Malawi wameanzia kati kipindi cha pili

64' Malawi wanafanya badiliko la wachezaji

65' Mpira wa adhabu kulekea lango la Taifa Stars baada ya Himid Mao kumchezea ndivyo sivyo mchezaji wa Malawi

67' Tanzaniawanakosa goli la tatu baada ya kipa wa Malawi kufanikiwa kuutoa

68' Tanzania wamefanya badiliko la wachezaji

74' Tanzania wanapata kona pacha lakini zote hazijazaa matunda

90+4' Mpira umeisha na matokeo Tanzania 2-0 Malawi

Last edited by a moderator:
Twendeni mapema tukawasapoti vijana wetu!kwa pamoja inawezekana.
 
Hii game sijui km itaoneshwa live,myb azam wafanye yao tuone wa mikoanh....

Viva TAIFA STARS
 
Hii mechi wameidharau utashangaa tunapigwa au dro,mechi ya Nigeria taifa stars walijihami ndo maana ikawa dro hapa nashangaa kama wameridhika mno
 
Hii mechi wameidharau utashangaa tunapigwa au dro,mechi ya Nigeria taifa stars walijihami ndo maana ikawa dro hapa nashangaa kama wameridhika mno
Mkuu mechi ya taifa stars na Nigeria uliangalia mpira kweli!unawezaje kusema tulijihami!
 
Mkuu mechi ya taifa stars na Nigeria uliangalia mpira kweli!unawezaje kusema tulijihami!

Ilikuwa mechi tulicheza na kujituma maana tulikuwa tunacheza na anayejua,sasa naona hii ya Leo kama wengi wanaidharau hata wachezaji wanaidharau
 
tbc 1 huwa wanarusha mechi za taifa stars sa sijui kama na ya leo hii watarusha
 
Hii mechi wameidharau utashangaa tunapigwa au dro,mechi ya Nigeria taifa stars walijihami ndo maana ikawa dro hapa nashangaa kama wameridhika mno

he!!!!kumbe mpira umeanza!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…