Taifa Stars vs Uganda Cranes: Serikali yakabidhi tiketi 20,000 kwa TFF kwa ajili ya Mashabiki kuingia uwanjani

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
SERIKALI YAKABIDHI TIKETI ELFU 20 KWA TFF

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ndg. Saidi Yakubu amekabidhi tiketi Elfu 20 Kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)kwa ajili ya Mashabiki kuingia uwanjani kuishangilia Taifa Stars Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tiketi hizo, leo Machi 26, 2023 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Yakubu, amesema tiketi hizo zinajumuisha tiketi 7000 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tiketi 2000 za Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Tiketi 11, 000 za Wizara yake pamoja na wadau wa wizara hiyo waliounga mkono zoezi hilo.

" Tunamshukuru Rais kwa mchango wake katika Sekta ya Michezo, baada ya ushindi wa juzi ameongeza hamasa kwa kununua kila goli kwa shilingi Milioni 10, hili ni jambo kubwa, nawaomba Watanzania tujitokeze uwanjani tuishangilie timu yetu, wapate nguvu za kupata ushindi, amesema Katibu Mkuu Yakubu.

Taifa stars itacheza mchezo wa marudiano na Uganda The Cranes Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mchezo wa awali waliibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 mchezo uliochezwa katika mji wa Ismailia nchini Misri.

IMG-20230326-WA0929(1).jpg

IMG-20230326-WA0944(1).jpg
IMG-20230326-WA0928(1).jpg
 
IMG-20230326-WA0130.jpg
IMG-20230326-WA0129.jpg
IMG-20230326-WA0128.jpg
IMG-20230326-WA0131.jpg

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Attachments

  • IMG-20230326-WA0130.jpg
    IMG-20230326-WA0130.jpg
    87.5 KB · Views: 2
Watanzania hawapendi mpira

Watanzania maneno mengi, uwanjani hawaendi hadi wabustiwe kama mashoga

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Ukweli watanzania hawapendi mpira ila wanazipenda simba na yanga tu. Angalia mechi ya Kagera dhidi ya Coastal union unakuta watazamaji hawazidi hata 500 lakini ikiwa dhidi ya simba au yanga wanafika hadi 15000.
 
Naangalia hapa mechi ya Ukraine na England watu wamelipa bei ya chini 48,000

Na uwanja umejaa

Watanzania bei ya 3000 ila hawaendi uwanjani na hawajazi

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hapa hata wakisema watu waingie bure uwanja hauta jaa, Mechi za Simba na Yanga watu wengi wanatoka mikoani
 
Back
Top Bottom