30 August 2018
Dar es Salaam, Tanzania
Wachezaji wote wa Taifa Stars wakiwemo wale walioitwa kuchukua nafasi ya wachezaji waliotimuliwa wa Simba SC, wameanza rasmi mazoezi chini ya Kocha Emmanuel Amunike leo jijini Dar-es-Salaam.
Kocha Amunike toka Nigeria, aliwahi kuzitumikia kama mchezaji kwa mafanikio makubwa timu ya taifa ya Nigeria na timu kadhaa za kubwa barani Ulaya ikiwemo ya Barcelona.
Emmanuel Amunike hakuwa mchoyo kuzungumzia filosofia yake ya kwanza ktk mazoezi ya jinsi ya 'timu na mchezaji' kumiliki mpira kwa manufaa ya timu kulinda na kupata ushindi.
Kocha ameonesha kuridhishwa na mapokeo ya mafunzo kwa wachezaji na ari yao ya kufanya mazoezi na hivyo kuwa na matumaini makubwa ya timu kufanya vizuri.
Source : MCL digital
Wadau wengi wa soka wamesema, ujio wa Amunike ni fursa kwa wachezaji wa ndani Tanzania kuongeza bidii, nidhamu ndani na nje ya viwanja na kufuata maelekezo ya kocha huyo mpya ili wapate kuwa wachezaji wa kimataifa kama Mbwana Samatta, Simon Msuva kwa kuwataja kwa uchache.
Fursa hiyo ni kutokana na Emmanuel Amunike kufahamika kimataifa na mtandao wake ktk ulimwengu wa soka basi wachezaji wa-Kitanzania wakisikiliza,kujifunza, kufanya mazoezi kwa bidii bila shurti wanaweza kuunganushiwa ulaji ktk timu kubwa barani Afrika, Ulaya na Marekani.