Taifa Stars waenda Cape Verde bila Dreamliner

October 9, 2018
Dar-es-Salaam, Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania – Taifa Stars kitaondoka usiku wa leo kuelekea mjini Praia, Cape Verde kwa ndege ya kukodi kuifuata timu ya taifa ya huko kwa ajili ya michuano ya kufuzu kwa michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kambi ya timu hiyo Waziri Mwakyembe amesema, mabadiliko ya safari hiyo kutoka Dream Liner na kuamua kukodi ndege yanatokana na ufinyu wa uwanja wa ndege wa Mjini Praia ambao hauwezi kutua ndege kubwa. Aidha Waziri Mwakyembe amewataka wachezaji wa Taifa stars wakacheze kwa kujituma ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo huku akiwasihi watanzania kuiombea timu hiyo. Kwa upande wake Rais wa TFF Wallace Karia na Nahodha Msaidi wa Taifa Stars Himidi Mao wameelezea maandalizi ya mchezo huo.
Hawa watu kwanini huwa hawawezi kusema ukweli?
 
wameshituka uchumi na sifa za kijinga !!!wangekubal tu kwamba hicho kiwango cha dola 2000/1500 kwa maisha ya mtanzania wa sasa ni kubwa mno!!isingewezekana ndege ya watu 262 ijaye!!watu wamekosekana na si busara kupeleka ndege kubwa hivyo!!ni uungwana tu ,kuliko kuanza mala run way ni fupi
Watu wanaogopa kukata maana wakirudi watadaiwa kodi/ au watafufuliwa kodi za zamani
 
Kwani walijuwa wataenda na dream liner ?????
 
Cheki madege makubwa uwanja wa kimataifa wa Cape Verde kwa jina la Praia Nelson Mandela airport ikiwemo hili la shirika la ndege la Cape Verde, Cabo Verde Airlines. Uwanja wa kimataifa wa Cape Verde ulipanuliwa mwaka 2012 na kuwekewa vifaa vya kisasa kuhudumia ndege zote kubwa pamoja na ongezeko la abiria kutokana na kisiwa hicho kuwa kivutio kwa utalii wa kimataifa.
Ukiwa na watawala waongo kwa kiwango hiki Nchi inaumia Sana Kitu sijaelewa Hawa watu wanadhani marufuku zao kuhusu media wanadhani wote tunaangalia tbc 1daah
 
Kwani bomberdier zipo wapi?au bado zipo matengenezo?
October 9, 2018
Dar-es-Salaam, Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania – Taifa Stars kitaondoka usiku wa leo kuelekea mjini Praia, Cape Verde kwa ndege ya kukodi kuifuata timu ya taifa ya huko kwa ajili ya michuano ya kufuzu kwa michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kambi ya timu hiyo Waziri Mwakyembe amesema, mabadiliko ya safari hiyo kutoka Dream Liner na kuamua kukodi ndege yanatokana na ufinyu wa uwanja wa ndege wa Mjini Praia ambao hauwezi kutua ndege kubwa. Aidha Waziri Mwakyembe amewataka wachezaji wa Taifa stars wakacheze kwa kujituma ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo huku akiwasihi watanzania kuiombea timu hiyo. Kwa upande wake Rais wa TFF Wallace Karia na Nahodha Msaidi wa Taifa Stars Himidi Mao wameelezea maandalizi ya mchezo huo.
Habari & Video kwa hisani kubwa ya:
Source: Global TV Online
 
Ashtakiwe kwa kutukana Airport ya watu mjinga mjinga uyu
 
Hivi hawa wanasiasa wanatuona sisi wote ni wajinga na mbumbumbu, swine
 
Back
Top Bottom