Taifa Stars wamefungwa kihalali

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
TAFAKURI NJE YA 18

Taifa Stars wamefungwa kihalali

Wamezidiwa mikakati kama ambavyo Stars waliweza kuwazidi wapinzani mikakati ya kimchezo katika games 3 na kunufaika

Hii ni michuano ya kufuzu World Cup

Standards are high
Kila mpinzani anajiandaa na kuna muda mechi inamnufaisha aliyejiandaa vyema na kufanyia kazi maandalizi

Sioni mahala pa kulaumu yoyote

Naiona Project ya Muda mfupi ya Kocha Kim Poulsen ilihitaji Support kubwa kuonyesha ushindani wa hali ya juu na soka la kiwango cha juu katika mechi ya Ugenini ili tupate tathmini endelevu kuandaa project ya Muda wa kati na mrefu

Tanzania ina kizazi bora sana muda huu kwa wachezaji chini ya miaka 25 mpaka U20.

Hawa wakiandaliwa ki professional kuelekea safari ya falsafa isiyotetereshwa na mechi moja tunaweza vuka daraja moja kwenda mbele.

Ndio projects endelevu kitaalamu na kitaalamu huandaliwa katika maono.

Niipongeze Serikali, TFF na wadau wakubwa kuonyesha Kushika mkono soka la Tanzania na wawekezaji.

Turudi katika maandalizi tu focus na michuano ijayo kuanzia sasa .

Hili ni daraja kwa tafakuri yangu.

Maana tofauti na kutoka katika mbio za Kufuzu World Cup Rasmi ila kuna mengi Positive tumeyapata na kutaonyesha katika michuano hii

Bado hatuna idadi ya kutosha ya Wachezaji professionals na wenye exposure ya soka la Kimashindano kinataifa.

Tuanzie hapa kwa vijana na Vitalu na falsafa na elimu .

MIMI NITABAKI KAMA SHABIKI WA KUGALAGALA WA TAIFA STARS NA WACHEZAJI WAVUJA JASHO WA TANZANIA KATIKA USHINDI NA KUPOTEZA.

NDIO SAFARI YA SOKA ILIVYO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…