Taifa Stars yachangiwa Bilioni 1.6 ili wafuzu kombe la dunia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania pamoja na wadau wa soka nchini kuungana kwa pamoja na kuhakikisha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa Miguu (Taifa Stars) inafanya vizuri kwenye michezo yote iliyobaki ili kufuzu kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022.

Ametoa wito huo leo (Alhamis, Novemba 4, 2021) wakati akiongoza Kikao cha pamoja cha wadau wa soka Nchini katika ukumbi wa uwanja wa Taifa wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Ambapo katika kikao hicho wadau wa Taifa Star wamechangia Shilingi Bilioni 1.6 ambazo zitatumika kuihudumia timu katika maandalizi ya mechi zilizobaki za kufuzu kombe la Dunia.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema ni lengo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anakuza sekta ya michezo nchini na anataka kuona mafanikio katika timu za Taifa hivyo mikakati ya kuifanya timu ya Taifa ifanikiwe ni sehemu ya kutimiza malengo ya Mheshimiwa Rais.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda, Taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau wengine kuendelea kujitokeza kuichangia timu ya Taifa ili iweze kuweka Historia ya kushiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Wadau Walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na GSM, TAIFA GAS, AZAM, CRDB, NBC, LAKE OIL, STAR OIL, K4 SECURITY, KAMBIASO pamoja na wadau wengine.

Chanzo: Michuzi Blog
 
Hii timu yetu huwa ina tabia moja,
Ukiipigia chapuo ukaisapoti , na kufuatilia mechi zake , ndio inafungwa sasa.
Ila ukiisahau na kuipuuzia, ukainyima uzito na tumaininla kusonga mbele ndio inafanya vizuri.
Sasa kwa hiki kilichofanywa na hawa wadau mpaka sasa mnajua kitakachotokea!
 
Mimi sio mtabiri wala nabii... Ila Taifa Stars kwenda Qatar 2022 ni Future Impossible Tense...

Serikali inatuona sisi mabwege sana..

Hivi haijui africa kuna nchi zaidi ya 50 zinagombea nafasi 5 tu za kuwakilisha africa world cup?

Taifa starz wanaanzia wapi kufuzu huku kina ghana, ivory coast, tunisia, algeria, morocco, nigeria, cameroon, egypt, na wengineo wengi nao wanazitaka hizo nafasi 5
 
Ukweli Mchungu...Unajua Huwezi from Nowhere ukataka Ushindi Uende Kombe la Dunia. Utatoka Tuu Kwenye Mtoano...Ukitaka Uliamini Hili...Tanzania hii Hakuna Timu Kuanzia Club mpaka Ya Taifa Inayoweza Kulinda Ushindi Mpaka Mwisho,Takwimu zinaonyesha Hakuna...Achana na Mifano Michache 2,3. Uzoefu ndio huo.
Mi Namwamini Mtu Mmoja Akiniambia Jambo Naamini sababu Linatoka Kwake, mfano Bondia,Riadha Kina Alphonce Simbu,Gerald Geaye,Failuna Matanga,nk nk,
Lakini Kwa Upande wa “Timu” bado Sanaaa kuwaamini. Watanzania Wanapenda sana Mpira,Ila Wanapenda Zaidi Matokeo[emoji3516][emoji851][emoji851][emoji12] tupo Kwenye kundi Rahisi tuu,Tukiingia Mtoano ndio tutajua hatujui[emoji41]
 
Safari kuelekea Kombe la Dunia

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassimu Majaliwa Kassimu leo Novemba 05,2021 ametembeam Kambi Ya Timu Ya Taifa (Taifa Stars).

Taifa stars itakutana na DRC Novemba 11,2021 uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam na Novemba 14,2021 itakutana na Magagascar Jijini Antananarivo.

Safari imeanza
Lazima tufike World Cup
 
Hizi ni habari za michezo au za siasa?
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania pamoja na wadau wa soka nchini kuungana kwa pamoja na kuhakikisha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa Miguu (Taifa Stars) inafanya vizuri kwenye michezo yote iliyobaki ili kufuzu kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022.

Ametoa wito huo leo (Alhamis, Novemba 4, 2021) wakati akiongoza Kikao cha pamoja cha wadau wa soka Nchini katika ukumbi wa uwanja wa Taifa wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Ambapo katika kikao hicho wadau wa Taifa Star wamechangia Shilingi Bilioni 1.6 ambazo zitatumika kuihudumia timu katika maandalizi ya mechi zilizobaki za kufuzu kombe la Dunia.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema ni lengo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anakuza sekta ya michezo nchini na anataka kuona mafanikio katika timu za Taifa hivyo mikakati ya kuifanya timu ya Taifa ifanikiwe ni sehemu ya kutimiza malengo ya Mheshimiwa Rais.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda, Taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau wengine kuendelea kujitokeza kuichangia timu ya Taifa ili iweze kuweka Historia ya kushiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Wadau Walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na GSM, TAIFA GAS, AZAM, CRDB, NBC, LAKE OIL, STAR OIL, K4 SECURITY, KAMBIASO pamoja na wadau wengine.

Chanzo: Michuzi Blog
Hizo hela si bora hata wangewakopesha wamachinga kwa riba ya 10%, kuliko kwenda kuzichoma moto 🔥!!!!
 
Baada ya makato ya miamala Sasa wamehamia kwenye michango ya stazi
 
Just like that! aliewaambia ili kufuzu kombe la dunia inahitajika michango akapimwe mkojo.
 
Wachezaji wa simba na yanga.. watupeleke world cup kweli?

Yaani foward john boko na fei toto kiungo wakacheze world cup kweli kwa kufuzu kihalali kabisa
 
Labda anazungumzia world cup ya Ruangwa.
 
Serikali inatuona sisi mabwege sana..

Hivi haijui africa kuna nchi zaidi ya 50 zinagombea nafasi 5 tu za kuwakilisha africa world cup?

Taifa starz wanaanzia wapi kufuzu huku kina ghana, ivory coast, tunisia, algeria, morocco, nigeria, cameroon, egypt, na wengineo wengi nao wanazitaka hizo nafasi 5
Hao ndo wenye nafasi zao.wengine ni wasindikizaji tu.mwaka 2015 tulijitutumua tukapangwa na algeria wakatupiga goli 7.Ilikua balaa.Mtifuano mwingine uko Amerika ya kusini ila napenyewe kuna wenye nafasi zao.Tatizo hatutaki kuwekeza vyakutosha alafu tunataka mafanikio makubwa kwa mipango ya zima moto kitu ambacho hakiwezekani.
 
Back
Top Bottom