Ndugu zangu binafsi hile mechi niliicheki tokea kuzindua uwanja mpaka mchezo unaisha,yafuatayo niliyaona;
uwanja wao unafanana na wetu kwa kiasi kikubwa japo wao haujafunikwa wote, katika kuzindua wenzetu walifanya kweli, waliandaa mpaka mashindano ya mbio, hotuba zilikuwa za kumwaga, wakati wa halftime wanariadha walizunguka mbio (100m&200), waliwasha mafataki uwanja mzima (kama S.A 2010 world cup), n.k baada ya hapo niliwaza sana huku kwetu TFF mbona haikuandaa haya ama ndo low creativity? for sure TFF haikutenda haki kwa uwanja wetu na kwa watanzania
kimchezo wapiganaji wetu wengi hawakuwepo, baada ya Ndihire kuchomwa mshale aliingia Kaseja naye akachomwa jingine,mabeki wetu walijisahau sana,mastriker wetu walishindwa kujipanga pasi zikawa zinaishia kwa mabeki
nadhani tunahitaji kutengeneza vijana zaidi yawezekana hawa wa sahivi wamechoka na hawana tena uwezo wa kutumia mbinu mpya