Taifa Stars yanyakua dola 10,000 baada ya kushika nafasi ya 3 COSAFA

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
TANZANIA imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya COSAFA Castle baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Lesotho kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku huu Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.

Shujaa wa Taifa Stars leo amekuwa golikipa Said Mohammed Mduda aliyepangua penalti ya Nahodha wa Mamba, Thapelo Mokhehle baada ya Sera Motebang kugongesha mwamba wa kulia mkwaju wake na kurudi uwanjani.

Waliofunga penalti za Lesotho ni Hlompho Kalake na Tsoanelo Koetle wakati Shiza Kichuya aligongesha mwamba wa juu penalti ya kwanza ya Tanzania, kabla ya Nahodha Himid Mao,Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Daudi kumtungua kipa wa Mamba Samuel Ketsekile kuipatia Taifa Stars ushindi mzuri wa 4-2.

Nahodha wa Tanzania, Himid Mao (kulia) akiweka mpira kifuani mbele ya kiungo wa Lesotho, Napo Matsoso (kushoto) leo Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini

Kipa Said Mohammed amepangua penalti ya Nahodha wa Lesotho, Thapelo Mokhehle kuipa Tanzania ushindi wa tatu COSAFA
Ushindi unakuja siku 25 baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 Juni 10, mwaka huu katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi L kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Romeo Kasengele wa Zambia, aliyesaidiwa na washika vibendera Thomas Kusosa wa Zimbabwe na Helder de Carvalho wa Angola, ndani ya dakika 90 timu hizo zilishambuliana kwa zamu, Lesotho wakitawala zaidi kipindi cha kwanza na cha pili Taifa Stars wakazinduka.

Kutoka na ushindi huo, Tanzania inaondoka na dola za Kimarekani 10,000 zaidi ya Sh. Milioni 22 kwa fedha za nyumbani, wakati Lesotho wamepata dola 8,300.

Fainali ya COSAFA Castle 2017 itachezwa Jumapili Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng mjini Rusternburg baina ya majirani, Zambia na Zimbabwe na bingwa atapata dola 42,000 na mshindi wa pili dola 21,000.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Said Mohammed, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Nurdin Chona, Salim Mbonde/Abdi Banda dk61, Salmin Hoza/Muzamil Yassin dk61, Himid Mao, Simon Msuva, Raphael Daudi, Stahmili Mbonde/Elias Maguri dk71 na Shiza Kichuya.

Lesotho; Samuel Ketsekile, Itumeleng Falene, Motlomelo Mkwanazi, Thapelo Mokhehle, Bokang Sello, Kefuce Mahula/ Hlompho Kalake dk89, Tumelo Khutlang, Tsoanelo Koetle, Napo Matsoso, Jane Ntso/ Mabuti Potloane dk59 na Sera Motebang.
 
Hongera.Pamoja na kufanya vizuri sijasikia serikali ikiwapongeza.hizo hela wagawane tu! by the way nilipokuwa naangalia niliona kama South africa wakipewa kitu kama ngao ya hisani baada ya kuifunga namibia,wakati hata mshindi wa tatu hatukupewa chochote zaidi ya medali.ile ilikuwa nn? sikuelewa.Halafu medali tumezoea kuona ya mshindi 1-gold,2-silver na 3-bronze.Sasa pale zilitolewa mpk mshindi wa ngapi?na zilikuwa za aina gani?
 
$ 10,000 sawa na Tshs 22,000,000/= du sasa hapa watagawana ngapi ngapi sasa! Wakati Malinzi alikua wanachota USD 10,000 peke yake, team ya taifa stars yenye wanasoka zaidi ya 20, bench la ufundi,kamati ya ufundi,Dr wa team, hapa wanafika 30! Zen ndo wagawane hizo 22,000,000 walahi soccer la bongo haliwezi fika popote!
 
Hongera.Pamoja na kufanya vizuri sijasikia serikali ikiwapongeza.hizo hela wagawane tu! by the way nilipokuwa naangalia niliona kama South africa wakipewa kitu kama ngao ya hisani baada ya kuifunga namibia,wakati hata mshindi wa tatu hatukupewa chochote zaidi ya medali.ile ilikuwa nn? sikuelewa.Halafu medali tumezoea kuona ya mshindi 1-gold,2-silver na 3-bronze.Sasa pale zilitolewa mpk mshindi wa ngapi?na zilikuwa za aina gani?
Baada ya bronze labda wakatoa medali ya bati au ya plastic kabisa
 
Huoni kama nikipmo cha ku-Improve kisoka? Au ww kwa akili zako unajua nn? Walioweka hivyo viwango hawana akili au ww ndo huna akili?
 
Hongera.Pamoja na kufanya vizuri sijasikia serikali ikiwapongeza.hizo hela wagawane tu! by the way nilipokuwa naangalia niliona kama South africa wakipewa kitu kama ngao ya hisani baada ya kuifunga namibia,wakati hata mshindi wa tatu hatukupewa chochote zaidi ya medali.ile ilikuwa nn? sikuelewa.Halafu medali tumezoea kuona ya mshindi 1-gold,2-silver na 3-bronze.Sasa pale zilitolewa mpk mshindi wa ngapi?na zilikuwa za aina gani?
Haya ni mashindano ya southern countries wewe umekaribishwa tu kama mgeni mualikwa ishu ya tuzo ,ngao haikuhusu
 
Utawala wa Magufuli umejaa neema.

Hadi Taifa Stars imeshinda
 
TANZANIA imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya COSAFA Castle baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Lesotho kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku huu Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.

Shujaa wa Taifa Stars leo amekuwa golikipa Said Mohammed Mduda aliyepangua penalti ya Nahodha wa Mamba, Thapelo Mokhehle baada ya Sera Motebang kugongesha mwamba wa kulia mkwaju wake na kurudi uwanjani.

Waliofunga penalti za Lesotho ni Hlompho Kalake na Tsoanelo Koetle wakati Shiza Kichuya aligongesha mwamba wa juu penalti ya kwanza ya Tanzania, kabla ya Nahodha Himid Mao,Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Daudi kumtungua kipa wa Mamba Samuel Ketsekile kuipatia Taifa Stars ushindi mzuri wa 4-2.

Nahodha wa Tanzania, Himid Mao (kulia) akiweka mpira kifuani mbele ya kiungo wa Lesotho, Napo Matsoso (kushoto) leo Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini

Kipa Said Mohammed amepangua penalti ya Nahodha wa Lesotho, Thapelo Mokhehle kuipa Tanzania ushindi wa tatu COSAFA
Ushindi unakuja siku 25 baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 Juni 10, mwaka huu katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi L kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Romeo Kasengele wa Zambia, aliyesaidiwa na washika vibendera Thomas Kusosa wa Zimbabwe na Helder de Carvalho wa Angola, ndani ya dakika 90 timu hizo zilishambuliana kwa zamu, Lesotho wakitawala zaidi kipindi cha kwanza na cha pili Taifa Stars wakazinduka.

Kutoka na ushindi huo, Tanzania inaondoka na dola za Kimarekani 10,000 zaidi ya Sh. Milioni 22 kwa fedha za nyumbani, wakati Lesotho wamepata dola 8,300.

Fainali ya COSAFA Castle 2017 itachezwa Jumapili Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng mjini Rusternburg baina ya majirani, Zambia na Zimbabwe na bingwa atapata dola 42,000 na mshindi wa pili dola 21,000.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Said Mohammed, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Nurdin Chona, Salim Mbonde/Abdi Banda dk61, Salmin Hoza/Muzamil Yassin dk61, Himid Mao, Simon Msuva, Raphael Daudi, Stahmili Mbonde/Elias Maguri dk71 na Shiza Kichuya.

Lesotho; Samuel Ketsekile, Itumeleng Falene, Motlomelo Mkwanazi, Thapelo Mokhehle, Bokang Sello, Kefuce Mahula/ Hlompho Kalake dk89, Tumelo Khutlang, Tsoanelo Koetle, Napo Matsoso, Jane Ntso/ Mabuti Potloane dk59 na Sera Motebang.
Hiyo hela ni kubwa sana kwa uwezo wao kimpira,,,na inatosha kabisa..Wangetaka vikubwa wangefanya makubwa,,siyo kila siku sisi ni kujitahidi tuuu..
 
Ushindi finyu Ila hongera mwanzo mzuri
 
Back
Top Bottom