hahaha, ungejua huyo JK unaemsifia ameajiriwa na wananchi wa Tz, kuanzia mkulima hadi mfanya kazi, usingesema vijana wa JK. Hao ni vijana na watoto wa watz. Usiwe unampa masifa Raisi awaye yote yule kama vile yeye ni mfalme mteule. Kwa miaka ya siku hizi za uelewa, Rais wetu ni Muajiriwa tu ambaye sisi tumemwamini na kumkabidhi majukumu makubwa ya kuongoza nchi. Ndo maana lazima anatakiwa kuwa accountable kwa wananchi wake. bila wananchi huyo JK angepata wapi kibarua?hujui kama kodi zetu ndo zinazomfanya aishi?Kodi anayokatwa hadi mtoto wako kwa VAT akinunua pipi...., ndo inayomfanya yeye apande ndege na kutuwakilisha kufanya yale majukumu ya juu. kuna siku kibarua kitaisha. Kwahiyo, watu wenye Rungu la kupata sifa za nchi yetu, sio mwajiriwa, ni Mwajiri ambae ndo sisi watz wote. Tunatakiwa kuwa proud wote kwa pamoja, sio kumpa sifa mtu mmoja kwavile tu yeye ni rais. Kama uongo, we subiri kinyang'anyiro kijacho, utakavyoona anavyojikomba kwa wananachi ili tumwajiri kwa miaka mingine mitano. hapo ndo utajua kuwa WANANCHI NDO WASHIKA RUNGU. na wananchi ndo wamiliki wa vitu vyote.
Hongera sana Taifa stars. lakini nawapeni pole, nasikia mmepata shida sana kule uganda, viongozi wa FUFA hawajawatendeeni vyema kama sisi tulivyowafanyia wao hapa. pia, nasikia kuna mashabiki wetu wengine waliumia, na mwanafunzi mmoja wa Kampala mtz. poleni na viongozi pia. Mi nilifikiri Mpira huu kwa waganda ndo ungeonyesha namna gani wao ni watu wanaowajali watz, ili kupromote Huo muungano wanaoulilia. sasa kama hata kukiwa na muungano, MBONA KUTAKUWA NA UUGANDA, UTANZANIA, NA UKENYA, UBURUNDI, NA URWANDA. tusije tukaishia kusuluhisha matatizo kama ya Pemba. Esalaleee...hahaha.