Shetani ana hila, ni mjanja mjanja, ana ya jua maandiko, ana wajua hao manabii wengine wote. Shetani ana tambua hao manabii wote walitumwa na Bwana Yesu/Mungu kuja kufanya kazi zake kwa wanadamu pia kuwaletea ujumbe wa Mungu/Bwana Yesu.
Kwa nini Yesu? BWANA YESU ndiye MUNGU. Alipo kuja duniani alikuja kuutimiliza ule unabii wote alio watuma hao ulio waita manabii wengi. Yesu alikuwa ni game changer ni Mungu mwenyewe, ndiye Focal personal , ndiye Mungu tunaye mtafuta siku zote kwa kumuomba, kumtolea sadaka na kumtegemea. Shetani akishindwa kufanikiwa kuvuruga ukweli huu kuwa Bwana Yesu ni Mungu aliye uvaa uwanadamu akaishi kati ya wanadamu aka wafundisha jinsi ya kuwa wafuasi wake, basi shetani ajua kabisa hana chake tena/ kaisha.
Lakini sijui hata hao manabii wengine kama watu wana elewa vizuri kwa nini Bwana Yesu/ Mungu aliwaleta hapa duniani?
Mfano ni Yohana Mbatizaji, kuna mh mmoja anapenda kumtolea mfano na kwa kumuita jina la Quran (sina hakika -Yunusi na dhani). Anasema, "Alikuja kama mtangulizi wa kumsafishia njia Bwana Yesu." Ndio ni kweli ndivyo Biblia inavyo sema na hata yeye Yohana mbatizaji kabla ya ujio wake hapa duniani, Mungu aliwatuma.manabii wakaleta ujumbe kwa wanadamu kuwa kabla Bwana Yesu/ Mungu kuja duniani kutakuwa na mtangulizi wake wa kumsafishia njia. Mama yake na Yohana Mbatizaji ni ndugu wa Mariamu mama wa Yesu. Malaika Gabrieli alitumwa kwa Mariamu na Elizabert Mama wa Yohana Mbatizaji kwa wakati mmoja.
Sasa tatizo ni kwa nini Yohana Mbatizaji kwa nini kusafishiwa njia kwa aliyemtuma? Je kuna nabii mwengine kabla ya Yesu alisha safishiwa njia? What is so special kwa Yesu mpaka asafishiwe njia?, kwa nini manabii kibao kuanzia Musa walitabiri ujio wa Yesu? Utapata jibu, Bwana Yesu ni Mungu na kuja kwake hapa duniani ni kukamilisha/hakiki kazi alizo kuwa amewatuma manabii wake kwa watu wake duniani inayo lenga ukombozi wa wanadamu. Na kusema kweli Bwana Yesu aliikamilisha kazi ya ukombozi wa mwanadamu kutoka katika hukumu ya kifo iliyo sababishwa na dhambi. Ndio alishinda dhambi na kifo.
Lakini nini maana ya kusafisha/kutengeneza njia? Kwa nini Yohana Mbatizaji abatize kwa maji, kabla yake kuna nabii mwengine yeyote alibatiza kwa maji?
Yohana mbatizaji alikuwa ana wandaa wanadamu kisaikolojia kuwa Bwana Yesu atakapokuja ana kuja na Agano jipya (A very New Covenant). Hilo agano litaingiwa kati ya Mungu/Bwana Yesu na wanadamu wote ulimwenguni. Agano hili ni ubatizo. Ubatizo ulioanzishwa kwa maji na Yohana mbatizaji na kukamilishwa kwa uvatizo wa Roho wa Mungu na Mungu mwenyewe pale Bwana Yesu alipo batizwa na Yohana mbatizaji na Roho wa Mungu/ Roho Mtakatifu akashuka kama Huwa/Njiwa kutoka Mbinguni akatua mabegani mwa Yesu. Na sauti ikasikika kutoka mbinguni/ mawinguni ikisema, Huyu ndiye mwanangu mpendwa wangu ni naye pendezwa naye msikilizeni yeye." Hapa kwenye kubatizwa kwa Bwana Yesu tunaona pia nafsi tatu za Mungu zilijidhihirisha zote na waliokuwepo wali zishuhudia ingawa sina hakika kama walipata neema ya kuzitambua. Maana wange zitambua kuwa ndizo nafsi tatu za Mungu na ndivyo zinavyo fanyakazi leo hii kusingekuwa na utata wa utatu mtakatifu wa Mungu wetu/ Mungu wa Usrael. Na hili agano jipya la Bwana Yesu la ubatizo
Lakini tujiulize kama wewe si shetani au mfuasi wa shetani unawakubali vipi manabii na mafundisho yao na uamini kwamba waliletwa na mungu huyo unaye taka kutuaminisha una muamini lakini ukatae Utaifa wao na Taifa lao? Hata wakati mwingine wafuasi wako kujiapiza
kulifuta Taifa hilo na watu wake ambao ndio Mungu mwenyewe aliamua kwa utashi wake wawe ndio kizazi chao kitoe manabii wake.
Nimesoma kwa umakini sana hii post yako kwa kiasi fulani umeonekana una uelewa wa maandiko matakatifu japo huku ambatanisha hata kifungu kimoja,inahitaji uwe na "Roho mtakatifu" kuweza kuijua biblia vizuri au kufundishwa na mtu aliye na roho mtakatifu sababu yeye ndio mshauri/mfafanuzi wa karibu kwa yeyote mwenye nia ya kwenda mbinguni iko hivi....
1.YESU MUNGU
>Hii mada ya UUNGU wa Yesu ni miongoni mwa kipimo cha uelewa wa mkristo,"yule Yesu aliyezaliwa na bikira mariam HAKUWA MUNGU" lakini Mungu alikuwa ndani yake! kuna Yesu kabla ya Mariam kumzaa (
NI Mungu) na Yesu baada ya kufariki pale msalabani then siku ya tatu akafufuka (
NI Mungu) ila yule aliyekuwa kazaliwa na bikira mariam,aliyekuwa anazunguka na wale mitume 12,aliyekuwa anapita anahubiri miji yoote ya wayahudi,yule hakuwa Mungu! yule alikuwa na "Title" mbali mbali mfano "MWALIMU" "MWANA","MWANA WA ADAM","MCHUNGAJI","NABII" MWANAKONDOO" n.k...(naweza kuandika kitabu kuhusu hii maada ya Yesu na Umungu wake ila kwa sasa niishie hapa)
2.UTATU (TRINITY)
>Hii pia ni miongoni mwa hoja zilizowagawa wakristo ulimwenguni koote iliwahi ibuliwa na wakatoliki tangia karne ya kwanza!.Nimeona wewe umeigusia japo kidogo sana na hujaielewa,kimsingi hakuna neno TRINITY (UTATU MTAKATIFU) kwenye biblia ni maneno ya watu tu! wala hakuna mahala mitume wamembatiza mtu kwa jina la baba ,mwana na roho mtakatifu! hakuna mahala kwenye biblia utakuta watu wamebatizwa kwa huo utatu watu woote kwenye biblia walibatizwa kwa jina la YESU tu! na sio utatu,na Mungu kwa taarifa yako ni mmoja na hajagawanyika kwenye hizo nafsi tatu unazozisema wewe! "MUNGU NI MMOJA HAKUNA UTATU" wala hakuna mwingine pembeni yake HAKUNAAA (Kumb 6:4) Mungu ni mmoja! mwenyewe anakwambia ni Mungu mwenye wivu na usiwe na Miungu wengine iweje leo useme kuna mungu mwana,baba na roho mtakatifu????
3.TAIFA TEULE ISRAEL
>Hii maada niliwahi iandikia thread hapa JF baada ya kuona watu wengi hawajui kabisaa kabisa kuhusu hili taifa la israel nitaweka link chini ukaisome yoote ila kwa haraka nitajitahidi kuelezea historia fupi kuhusu hili taifa fake la israel la sasa na kuna maswali nitakuuliza.
-ni kweli manabii woote kwenye biblia walikuwa wana wa israeli ila taifa la israeli lipi unalolizungumzia wewe kama ni hili la leo lililopo pale mashariki ya kati
Taifa la israeli tangu linaundwa na kuingia pale kaanan lilipewa na Musa/Yoshua amri na mafundisho ya Mungu ya kufuata ili liendelee kudumu pale ndio hizi sheria za Musa(TORATI) na zilikuwa zinasimamiwa na "WAAMUZI then baadaye MANABII" (soma kumb 28.....kujua masharti ya wao kukaa pale kwenye nchi ya ahadi) ndiomaana walivyokuwa wanayakiuka haya masharti walikuwa wanachukuliwa utumwani(wanapigwa vitani) au Mungu alikuwa anawapiga kwa mapigo mbali mbali kwakuwa wamekiuka masharti ya kukaa pale then wakimkumbuka Mungu wao wanatubu then Mungu anawainulia Nabii/mwamuzi wa kuwarudisha tena kaanani na Mungu sio mwanadamu mpaka aseme uongo ndiomaana alikuwa anawaadhibu mara nyingi saana pindi wakikosea na alikuwa anawabariki saana pindi wakiwa wanatimiza Masharti yake ndivyo ilivyokuwa kuanzia enzi za Musa mpaka Yesu anakuja nahadi leo hii ili upate baraka za Mungu kuna masharti yake unapaswa kuyatimiza!!
Alipokuja Yesu duniani Wayahudi walimkataaaa! so walikiuka tena lile andiko la kumbkumbu la torati 28:... la kutokutiii maagizo yake Mungu na kuyashika, wao walimkataa wakamsulubisha msalabani wakamuua so WHATS NEXT?? Yesu aliwaambia hakuna jiwe litasalia hapo israel,watauliwa na upanga (VITA),Watachukuliwa mateka (utumwani)na Yerusalemu itakaliwa na MATAIFA mpaka Muda wa mataifa utakapo timia (LUKA 21:24)! haya maandiko yalitimia mwaka 70 baada ya YESU ambapo Yerusalemu ilivamiwa na mfalme TITUS na ikaharibiwa vibaya ikachukuliwa na mataifa na wayahudi wakasambaa duniani koote kama watumwa/mateka vile vile kama neno lilivyosemwa (hiki ndio chanzo cha wayahudi kusambaa duniani koote mpaka leo).
kwa karibia ya miaka 2000 hadi Mwaka 1948 kuna watu waliokuwa wanajiita wayahudi walikusanyana wakaunda Taifa kwa msaada wa waingereza wakasema ni taifa la israeli na wao wana wa israel
Nina maswali yafuatayo hapa chini
1.Unauhakika gani hao waliorudi hapo mwaka 1948 ni wana -waisraeli waliokuwepo pale kipindi cha Yesu(descendants)??
2.Una uhakika gani kuwa waliorudi pale kuwa ni WAYAHUDI?
3.Wayahudi walikuwa ni watu wa Rangi"people of colour" maana yake walikuwa weusi hata kuna manabii wengi tu katika biblia wamejitaja kuwa ngozi yao ni nyeusi mbona hawa waliorudi pale israeli leo hii ni WAZUNGU kabisaaaa!
4.Lini hawa wanaojiita wayahudi waliorudi pale israeli walitubu dhambi yao ya kumkana Masihi wa Bwana then Mungu akawapa nabii aliyewarudisha pale kama maandiko yanavyosema?
5.kuna wayahudi weusi tii wanapatikana zimbabwe (Lemba people) na Nigeria unawahusisha vipi na hawa wazungu waliopo pale israeli sasahv?
6.Yesu alivyokuja alifanya mabadiriko kutoka (israeli ya kimwili -hekalu) kwenda kwenye israeli ya kiroho (hekalu ni moyo wako) ndiomaana imeandikwa sisi ni hekalu la Bwana,sasa hilo neno kuwa israeli hii ya leo ni taifa teule umesimamia maandiko yepi?
7.iliandikwa wapi ukikubali maandiko ya hao mitume ukubali pia na Taifa lao?
kukusaidia wayahudi halisi walishagatawanywa pale israeli kitambo sana hawatarudi hadi yesu arudi mara ya pili
soma na link hii hapa chini upate uhalisia zaidi juu ya hili taifa fake la israeli na siri kubwa ya shetani dhidi ya kanisa na maandalizi ya kuja kumpokea mpinga kristo
Uhalisia wa taifa la Israeli