Taifa vs harambee stars

Je kuna tv stesheni yeyote inaonyesha? Mwenye data atupe wajameni.
 
Wadau wenzangu mliopo uwanja wa Uhuru, tunaomba mtupe yanayojiri hapo uwanjani. Matokeo? List ipo vipi? Vijana wetu wanaonekana kubadilika kwa mbinu mpya za Polsen?

Nawasilisha
 
ni live luningani au? tupeane taarifa wadau
 
Nimejaribu ku-tune luninga sioni hilo gemu likionyeshwa. wadau mliopo uwanjani tupeni taarifa basi.
 
Harambee Stars 1 - Taifa Stars 0

Dakika 20 zimepita
 
Full time score Stars 1 Harambee Stars 1, bao la Taifa Stars kasawazisha Mrisho Ngassa, wenzetu wako vizuri Mariga na Denis Oliech wameitesa sana ngome ya Taifa Stars,kwa kweli kocha mpya Poulsen bado ana kazi...
 
Chuji alicheza? vipi kiwango chake
 
Chuji alicheza na alitawala kiungo kwa ustadi mkubwa kwa kweli tulimiss sana mchango wake timu ya Taifa, bao la Kenya lilifungwa na mchezaji wa inter Milan McDonald Mariga kwa mpira wa adhabu..Pia tumebabwa kiaina maana Harambe Stars walipiga bao la 2lililotokana na mabeki wa Stars kujigonga gonga wenye na kujifunga ila kwa mshangao wa wengi refa akalikataa.
 
Kaka Habari Yako!!?..Samahani Naomba Nikusawazishe,Nilikuwepo Uwanjani Na Chuji Aliingia Dakika 10 Za Mwisho Ila Alicheza Vizuri Kwa Dakika Alizoingizwa,Na Pia Goal Lao Jamaa Lilikuwa Ni Foul Na Wala Si La Kujifunga Ni Oliech Ndie Alifunga Baada Ya Kipa Kado Kuuachia Mpira Aliokwisha Ukamata Na Yote Ni Baada Ya Huyo Oliech Kumpiga Na Mguu Wa Kifua Kipindi Alipoenda Kuuwahi Mpira.Kwenye Swala La Kupendelewa Hilo Toa,Ni Mistake Ya Mshika Kibendera Ambaye Hakuona Ngasa Km Alikuwa Offside Kwenye Goal La Kusawazisha.Kiukweli ALivyoingia Mgosi Ndio Game Ilichange Japo Alikosa Goal Ambalo Ukiambiwa Ukose Inakuwa Ngumu Kukosa.Kipindi Cha 2 Tulitawala Sana,Haswa Baada Ya Kuingia Yule Mtoto Mwenye Jezi namba 7 Na Beki Alieingia Baada Ya Yondani.Uhuru Selemani,Tegete Na Jabir Aziz Leo Walikuwa Nje Ya Kiwango Kabisa Sijui Walichokuwa Wanafanya Uwanjani Ni Kitu Gani??.Ni Hayo Tu!!
 

Goli la Harambee stars lilifungwa na MCDonald Mariga dakika ya 13 kwa mpira wa adhabu ndogo, na Chuji aliingia dakika ya 69 ya mchezo kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…