Taiwan yaungana na Marekani, yadai Huawei ni kirusi cha kichina, Trojan Horse, yadai wao walishaipiga marufuku toka 4G inaanza

Taiwan yaungana na Marekani, yadai Huawei ni kirusi cha kichina, Trojan Horse, yadai wao walishaipiga marufuku toka 4G inaanza

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Waziri wa digitali wa Taiwan amesema Huawei ni kirusi cha kichina au Trojan horse kutoka China na ni hatari kuitumia kwenye mfumo wa mawasiliano ya nchi

Waziri huyo ambae zamani alikua muiba taarifa za kimtandao ama kwa kimombo hacker anasema wao Taiwan walishaliona hilo la Huawei muda mrefu toka mfumo wa 4G ulipozinduliwa nchini humo na kuipiga marufuku Huawei isishiriki kwa namna yoyote ile

Taiwan imeipa kandarasi kampuni ya Sweden ya Errickson kutengeneza mitambo ya 5G nchini humo

Taiwan’s digital minister depicts Chinese telecom equipment as ‘Trojan Horse’ | Taiwan News
 
Ni wajinga tu wanacheza ngoma ya mabeberu hao sweden ndio malaika kwamba hawawezi kufanya udukuzi? Kama vipi wajenge mitambo yao ya 5G na wasiwe tegemezi.
Beggers cannot be choosers
 
Ni wajinga tu wanacheza ngoma ya mabeberu hao sweden ndio malaika kwamba hawawezi kufanya udukuzi? Kama vipi wajenge mitambo yao ya 5G na wasiwe tegemezi.
Beggers cannot be choosers
Ni kweli naona ni wajinga, hata india nao ni wajinga, canada, australia,uk,france etc....hebu tuone alliance wake wa karibu sana kama russia, cuba kama wao watamuunga mkono?
 
Kwa habari yako China hana rafiki kwa sasa hata wale waliokuwa na urafiki nae kwa nia ya kutaka kumuangusha Mmarekani wameshtuka mkuu
Naona ndugu wamekula kona mkuu hahaha maana naona Moscow kimya kabisa, hata Asia yenyewe ambapo ndipo alipo bado sijasikia muungaji mkono
 
Naona ndugu wamekula kona mkuu hahaha maana naona Moscow kimya kabisa, hata Asia yenyewe ambapo ndipo alipo bado sijasikia muungaji mkono

China wana sera yao nenda ulete iwe pesa, tecnologia, madini na bila kujali umepata wapi ama umeiba ama umepata kwa uhalali, wao wanavitaka bila kujali ww ni rafiki ama ni adui wao ni kukusanya tu basi.

Sasa marafiki zake wamestuka lakini very late, kama Russia Mchina alinunua ndege zake za kivita baadae akazitengeneza kama zilivyo lakini kabafilisha jina tu, sasa Russia amestuka ndio analialia sasa[emoji23][emoji23]
 
Huawei iliwahi kusema yeyote mwenye mashaka kuhusu telecom equipment zake, Huawei itawapatia SOURCE CODE ya equipmemt zifanyiwe uchunguzi wa kina kama zina an embedded subroutine program for spoofing attack on unsuspecting buyers/cliet specifically Govt agencies and officials.

Taifa la kwanza kuzifanyia uchunguzi mitambo ya mawasiliano ya Huawei walikuwa ni Wajerumani hawakukuta chochote chenye kuhashiria kwamba equipment za Huawei zina include programs za udukuzi among othtter things.

Taifa la pili kupewa SOURCE CODE kwa uchunguzi ilikuwa ni Uingereza nao vile vile never found a trojan horse or worm of any shape or form putting to rest American wild allegation - sio kwamba Uncle SAM hajui ukweli huu, bado yupo determined to throw a monkey wrench into Huawei Global telecom equipmemt sales kwa kumwaribia sifa na scare mongering kwa potential buyer wa Huawei 5G gem, kisa? wakose wote - watu wa ajabu sana hawa.
 
Waziri wa digitali wa Taiwan amesema Huawei ni kirusi cha kichina au Trojan horse kutoka China na ni hatari kuitumia kwenye mfumo wa mawasiliano ya nchi

Waziri huyo ambae zamani alikua muiba taarifa za kimtandao ama kwa kimombo hacker anasema wao Taiwan walishaliona hilo la Huawei muda mrefu toka mfumo wa 4G ulipozinduliwa nchini humo na kuipiga marufuku Huawei isishiriki kwa namna yoyote ile

Taiwan imeipa kandarasi kampuni ya Sweden ya Errickson kutengeneza mitambo ya 5G nchini humo

Taiwan’s digital minister depicts Chinese telecom equipment as ‘Trojan Horse’ | Taiwan News
Taiwan anaongea sana
 
Back
Top Bottom