Taj Mahal, Urithi wa dunia

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Taj Mahal (Kiajemi تاج محل‎ - tāj-maḥal, taji la mahali) ni jengo zuri la kaburi lenye umbo la msikiti mjini Agra (Uhindi). Mara nyingi huhesabiwa kati ya majengo mazuri duniani.


Taj Mahal.
Taj Mahal ilijengwa 1631 - 1648 kwa amri ya Shah Jahan aliyekuwa mtawala wa nasaba ya Moghul aliyetaka kumkumbuka mke wake mpendwa 1631 Mumtaz Mahal. Shah Jahan aliwaajiri mafundi 20,000 kutoka Asia ya Kusini na Asia ya Kati walioongozwa na Mwajemi Ali Fazal kutoka Afghanistan. Msanifu huyu aliunganisha sifa za ujenzi wa Uajemi na Uhindi.

Taj Mahal imekuwa shabaha ya watalii wengi na tangu 1983 imeandikishwa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.

Jengo liko hatarini kutokana na hewa chafu. Magari hayaruhusiwi kukaribia jengo katika duara ya kilomita 2. Hata hivyo gesi chafu na mvua asidi zinaendelea kula mawe yake.
 
Hiyo style ya majengo hayo nilikuwa nafikiri ni ya Kiarabu
 
Hii kitu Ilimponza Bwana Jela Wa FOX RIVER, Alitaka kufurahisha moyo wa Mkewe, Mhandisi Solfield akatumia mwanya huo huo kufanya mipango, Bwana Henry kwa Hasira akalivunjilia mbali..!

Umenikumbusha mambo ya Prison Break Mkuu Bujibuji , then Jana usiku kijana wangu kaona hili jina lako akacheka sana akaniuliza maana yake nini nikamwambia sijui.
 
Na me ngoja nitafute ex wa kumjengea ata kibanda
 
Bwana ehhh hili jina linatafsiri ndefu mno, kuandika kwenye simu siwezi. RELI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…