KakaKiiza
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 11,794
- 9,075
Miaka ya 80 Wazee wangu walisumbuliwa na mauzauza pia na maradhi yasiyoisha, Basi siku moja wakasikia kuna mganga ametoka Uganda anatumia (Amaembe)Mapembe sijui niite hivyo ila kwa wakazi wa Kagera watanielewa kwa haraka, Basi huyo mganga siku ya siku akaja kama saa tano usiku hivi, akaweka zana zake mimi nilikuwa mdogo kama 12yrs old, basi nikawa naona nikiwachumbani nilifukuzwa nikaambiwa nikae chumbani
Baada ya Nusu saa nikasikia mlio wa Gari kama Subaru nje na Taa za gari zinawaka kali sana na milango ya gari inafungwa! Mnaojua Subaru Mlio wake au Alteza, basi nikasikia Mganga akikaribisha kwa kiganda Nsanyuse kukuraba Jaja Muhanga Huyo mgeni aliyekuja na gari akajibu kwa sauti nzito sana! Mlango ulikuwa umefungwa basi zile nyimba au chekecha vilikuwa vinapita dalini mwisho likasema Ohhh kumbe kuna mtoto chumbani nimemuona kwa kiganda sasa!!
Sasa kulikuwa na ndugu yangu eti akajua yule mganga ndiye anatembea juu ya gari akataka ampapase kumbuka ni giza hakuna taa basi alinaswa kibao!na kupewa onyo kali na hilo lijamaa! lilipomaliza kazi yake likatoka nje likawasha gari na kuwasha taa na kufunga mlango wa gari likageuza kwa fujo na kuondoka kwa kasi!!
Yule mganga akawambia wawashe taa Wazazi wangu wakawasha taa na wakapewa maelekezo! Na mganga akafungasha na kuondoka alipokuwa akiishi! Nyumbani tukabaki kuulizana yule ni nani alikuja na gari!
Niliogopa asubuhi mimi nikaenda kutizama wapi gari imepita wala hakuna hata tairi ya baisikeli!
Kweli uchawi upo ila nasikia Uganda ni mambo ya kawaida sana! Tupe kisa chako!