MC Henjewele ndo anaburuza hapa mjini anajulia sherehe na si mtu wa kupapuka kama MPOKI
Mc kamoga Hudson,
natumain kwa namna moja au nyingine utakuwa umehudhuria sherehe/hafla katika jiji la Dar es Salaam, je ni ma-MC gani uchwara uliowahi kukutana nao shereheni na wakafanya sherehe kuwa mbaya kutokana na kuboa watu?
1. MC PILIPILI a.k.a ZAKAYO - hiki kijamaa kinalazimisha u-MC lakini hawezi huyu labda aende kwenye kupiga ngoma za kienyeji huko kwao DODOMA.
Dah,sijajua kama una kisa nae au vipi, au labda siku hizi uwezo umepungua (unajua tena maskini akipata)
ila kwa jinsi navyomjua huyu jamaa ni balaa, kuna kipindi tuliwahi kuwa na sherehe ya harusi na alikua MC na tulifanyia kwenye hotel moja hv inamilikiwa na wahindi, yaani mpaka wahindi wakawa wasimama madirishani kuangalia maana ilikua ni balaa.. ukumbi wote ulikua ni kelele mpaka maharusi kwa kucheka.
labda siku hizi hana upako au sijui kama bado ameokoka maana by then alikua mlokole mzuri tu