Taja tukio la ujambazi uliwahi kushuhudia au kusikia uelezee ilikuwaje!

Taja tukio la ujambazi uliwahi kushuhudia au kusikia uelezee ilikuwaje!

adden

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
7,033
Reaction score
15,638
habari mabwashee..
elezo kichwa cha habari.
kama katika matukio ya ujambazi nilishuhudia ni haya..

ilikuwa mwaka 2003 mwanzoni hivi.nilikuwa ndani ya costa kutoka moshi kuelekea arusha.kufika maeneo ya KIA costa ikasimama kupakia abiria ambao walikuwa masai 2 na jamaa mwingine 1.kwa haraka wale manjeree walitoka mererani wakielekea arusha.aliingia kwanza yule abiria kisha masai wakafatia.yulee jamaa akaenda kukaa siti ya mwisho kabisa wale masai wakakaa hapo mbele.kufika katikati ya kingori na kikatiti yule jamaa kule nyuma akaomba kushushwa lakini konda akagoma kwamba amna kituo apo.jamaa akaanza vurugu na makelele ashushwe ikabidi abiria wamwambie konda amshushe kuondoa kero.basi imesimama jamaa akaanza kujivuta kama bi arusi yaani anashuka kama ataki vile!wakati konda anamlazmisha ashuke araka tayari mbele ya kosta imepaki RAV4 ikabloki wakashuka jamaa na makoti kipolisi.wakamdaka jamaa pale mlangoni na makofi kibao..kwamba wee ndio jambawazi tunakutafta sana leo tumekupata taja wenzio wako wapi?!akaonyeshea wale masai pale.wakashushwa wote na masai wake wakaingizwa kwenye RAV4 dreva akaambiwa ole wako upige simu tutakuua!kumbe wale masai walikuwa na mawe wanaenda kuuza arusha.lile tukio ilikuwa la akili nyingi sana.
 
Mimi nilishuhudia tukio la wizi dukani kwa Calvin Uswaa pale stendi ya haice katikati Morogoro sidhani kama sasa bado ipo hiyo stendi na duka la Calvin kama bado lipo ilikuwa 2008 -2010 kama sikosei ni zamani kidogo. Tuliingia kwenye hiace pale rais wote. Hali ilikuwa msagulano.
 
Back
Top Bottom