Taja Uongo mkubwa ambao ushawahi kuambiwa enzi za utotoni!

Taja Uongo mkubwa ambao ushawahi kuambiwa enzi za utotoni!

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,120
Reaction score
24,667
Utotoni kulikuwa na mambo mengi tuliyokuwa tunaambiwa na wakubwa wetu lakini baada ya kukua, ndio tukaja kugundua ilikuwa ni uongo!
Binafsi mimi nilikutana na haya;
1. Ukifukia soda ardhini ukiiacha wiki mbili itamea halafu inazaa utachuma, nililpofukia tu wakaichimba na kuinywa🤣🤣🤣daah walah..
2. Ngurumo wakati wa mvua ilikuwa ni mapipa yanapigwa mateke na mungu, mvua ni maji yaliyomwagika kutoka kwenye hayo mapipa[emoji23][emoji23]kwa kweli walitushinda...
3.Mwenzio akijamba usipotema mate utaota meno matakoni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji38][emoji38]
4.Ukikalia mafiga unapata majipu kwenye makalio....
5.Ukilia usiku, sauti yako itachukuliwa na mashetani[emoji39][emoji23][emoji23]🤣

Hebu tiririkeni hapa uongo ambao ushaambiwa, tutoe stress kidogo....
 
Ukimruka alielala basi sharit umrudie kumruka tena la sivyo atakuwa harefuki.
 
1:radi inabamiza walio vaa nguo nyekundu,
2:ukifa bongo unazaliwa china
3:ukinyooshea kidole kabuli ni lazima uking'ate bila hivo kinaoza
 
Ukinyooshea makaburi kidole basi lazima uking'ate mpaka kitoe alama la sivyo usiku utafatwa na mizuka.

Ukisema uongo basi lazima ufe usiku, kwa hiyo nilikuwa naamini wanaokufa wote ni wale waliosema uongo. Hahaaa utoto raha sana

Ukimeza tunda ya ubuyu basi utaota mbuyu kichwani.
 
Back
Top Bottom